Majadiliano ya mtumiaji:Kamau27
Weka madaUhamiaji Haramu Marekani
[hariri chanzo]Uhamiaji Haramu Marekani
Uhamiaji ni jinsi ambavyo watu hutoka mahali walikozaliwa na kuanza maisha katika nchi ambayo hao sio wenyeji. Watu huhamia nchi mpya wakitafuta nafasi mpya au kazi bora au pia kuendeleza masomo yao.
Nani ni “Mhamiaji Haramu?” na Jinsi Ambavyo Maisha Yao ni Tofauti
Marekani kuna “wahamiaji haramu” 30,000, hawa ni watu ambao wamepititsha muda wao kuishi humu Marekani. Hii ina maana kwamba watu hawa hawana nyaraka sahihi zinazowakubalisha kuwa na makao huku Marekani. Weingi wao wamechagua kuishi huku kwa sababu wao hufanya kazi zinazolipa vizuri, ili waweze kusaidia jamii zao zilizo nchi zao za kuzaliwa, kama Kenya. Kwa mfano, inawezekana mtu fulani kutoka Kenya alikuwa mmoja wa watu bila nyaraka sahili kwa muda mrefu huko Marekani. Hakuweza kurudi Kenya kwa sababu alijua asingeweza kupata cheti, au visa, ya kurudi Marekai. Maisha yake huku itakuwa maisha ya utumwa kwa vile atakuwa akifanya kazi kichinichini. Atalipwa pesa kidogo kulingana na wafanyakazi wengine kwa sababu mkurugenzi atakaye kuwa amemwajiri atajua kwamba mtu huyo ni mhamiaji haramu. Kazi nyingi zinazofanywa na wahamiaji huwa kazi ngumu zinazohitaji nguvu za misuli. Kazi hizi zinahitaji wafanyakazi wawe waangalifu sana kwa vile wakiumia kazini, hawana bima ya afya kuwalipia muswada wa hospitali. Kulingana na uchapishaji wa Ofisi ya Kumbukumbu ya Watu huku Marekani “ukosefu wa hali ya kisheria ya wahamiaji wengine, uwezo wa chini wa Kiingereza, elimu ya chini, na nafasi ndogo za kazi zina jukumu.” Kulingana na kauli hii, tunaweza kuelewa kwa nini wahamiaji wanalazimishwaa kufanya kazi zinazowahamu. Hawawezi kuchagua kazi wanazofanya kwa sababu kazi hizo ni chache na wanahitaji pesa za kutumia jamii zao nyumbani kwao.
Kizazi cha pili cha “wahamiaji haramu"
Mara kwa mara, athari inayohusu uhamiaji huathiri watoto wa wahamiaji. Hawa watoto hujipata katika hali ya mshangao kwa vile hawaielewi hali yao hapa Marekani. Jamii nyingi za Marekani hufikiri kuwa wahamiaji wamekuja kuzifanya kazi zao ndio maana vituo vya habari huzungumza kuhusu wahamiaji wakitumia uhalifu wa chuki. Jambo wanalosahau, ni kwamba watoto pia hutazama habari hizo na wanaweza kujihurumia wakiona vile wanavyochukuliwa na jamii zao. Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Sera ya Uhamiaji ilionyesha kuwa “Wanafunzi wahamiaji wanasema kwamba walimu wana matarajio ya chini yao, mara nyingi wanafikiri Kiingereza chao kuwa maskini. Wanaripoti kuwa walimu hufikiri kwamba watoto hawa wanaleta tabia mbovu shuleni.” Hapa tunaona mambo mawili yanayowaadhiri watoto wa wahamiaji; kwanza, walimu hawana imani kwamba watoto hawa wanaweza kuwa werevu kama watoto wengine darasani. Fikira hizi, hufanya watoto kujiona hafifu shuleni. Pili, tunaona jinsi walimu wanatarajia watoto hawa kuwa watoto wanaopenda vurugu. Watoto hawa wanatarajiwa kuleta vita shuleni kwa sababu ya kuwa wametoka familia za wahamiaji. Fikira hizi hufanya watoto wasiweze kufaulu shuleni kwa vile wanajiona kama wako chini ya watoto wengine. Ubaguzi huu, hueendelea kuwasumbua watoto hawa hata baada ya kumaliza elimu yao. Wana uoga huu wa kujiona kama hawastahili kuwa katika nchi hii. Wakati mwingine, uoga huu huhifadhiwa mpaka kizazi cha pili cha wahamiaji hawa.
Jinsi Wahamiaji Wanaendelea Kujikakamua
Ijapokuwa maisha ya wahamiaji huwa na matatizo mengi, bado wanaweza kufaulu licha ya haya yote. Wengi wa kizazi cha pili, wanaweza kujiendeleza maishani na kuwasaidia wazazi wao. Elimu ya Juu imewezesha wahamiaji kupata kazi zinazolipa fedha zinazotosha. Pia, kufanya kazi kwa bidii kumewezesha kizazi cha pili kufauli kama vile wazazi wao walivyoahadia. Watoto wengi wa wahamiaji wanaozaliwa Marekani wanasema kuwa wanajihisi kuwa Wamerika. Hii ina maana kwamba wanajiona kuwa wanastahili kuishi maisha ya Kimarekani. Kulingana na utafiti wa Mfano wa Watoto Wazima wa Wahamiaji, watoto wa kizazi cha pili wana elimu ya juu, wanaishi makao mazuri na mapato yao ya kila mwaka ni mengi luliko ya kizazi cha kwanza. Utafiti, huu unaonyesha kwamba baada ya kuishi Marekani wahamiaji wanaweza kuboresha maisha yao.
Kumbukumbu
[1] [2] [3]
[4]
[1]"U.S. Kuhudhuria Wahamiaji wa Kenya 30,000 wasiokuwa na sheria. "Uhamasishaji wa Umoja wa Mataifa 30,000 Wahamiaji wa Kenya wasio na sheria ~, wwwamadpocinsider.blogspot.com/2013/08/us-hosting-30000-illegal-kenyan_27.html.
[2]" Watu wa Diaspora Tofauti nchini Marekani." Migrationpolicy.org, 11 Agosti 2015, www.migrationpolicy.org/research/select-diaspora-populations-united-states.
[3]"Wamarekani wa Pili Wazazi". Mradi wa Utafiti wa Pew wa Jamii na Wavuti, 7 Februari 2013, www.pewsocialtrends.org/2013/02/07/second-generation-americans/.
[4] Zuehlke, Eric. “Immigrants Work in Riskier and More Dangerous Jobs in the United States.” Population Reference Bureau, Nov. 2009, www.prb.org/Publications/Articles/2009/usimmigrantsriskyjobs.aspx.