Majadiliano ya mtumiaji:JEBRA KAMBOLE

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jebra Kambole ni Mwanasheria Kijana na Wakili Maarufu Nchini Tanzania,


Historia ya Maisha yake


Kijana huyu alizaliwa tarehe 26 Juni 1987 katika mtaa wa Ipogoro Iringa Mjini, Mama yake anaitwa Coletha Ndelema na Baba yake ni Cunbert Kambole. Alianza darasa la kwanza mwaka 1995 na kumaliza mwaka 2001. Baada ya kumaliza elimu ya msingi alifaulu na kuchaguliwa kujiunga na Shule ya sekondari ya umma iitwayo Shule ya Sekondari ya Mazoezi Klerruu iliyopo Iringa mjini ambapo alisoma masomo ya sekondari kati ya mwaka 2002 mpaka mwaka 2005. Jebra Kambole alipata ufaulu mzuri na kuchaguliwa kujiunga na shule ya sekondari ya umma ya Njombe iliyopo Wilaya ya Njombe mkoani Njombe kwa masomo ya juu ya sekondari, yaani kidato cha tano na sita kuanzia mwaka 2006 mpaka mwaka 2008. Baada ya kumaliza kidato cha sita, alijiunga kama mwalimu katika Shule ya Sekondari Kitwiru wakati akisubiri matokeo ya mitihani ya kidato cha sita. Matokeo yalitoka Kijana Jebra Kambole alipata ufaulu mzuri kwa kupata alama A kwa somo la lugha ya kiingereza na kiswahili.Kwa matokeo hayo kijana alichaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam Kitivo cha sheria ambapo alisoma kuanzia mwaka 2008 mpaka mwaka 2012, Akiwa chuoni kijana huyu alifanikiwa kushiriki mashindano mbalimbali ya kimasomo hapo chuo na baada kukiwakilisha chuo katika mashindano ya afrika(PAN-AFRICAN MOOT COURT ON INTERNATIONAL HUMANITARIAN LAW) mwaka 2011 na Mwaka 2012 aliwakilisha vyema chuo kikuu cha Dar-es-salaam katika mashindano ya dunia kwa wanafunzi wa sheria nchini South Africa Johannesburg (JEAN PICTET MOOT COURT ON INTERNATIONAL HUMANITARIAN LAW).Baada ya kumaliza shahada ya sheria alijiunga na shule ya sheria Tanzania (the Law School Of Tanzania) kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia 2013 mpaka 2014 ambapo alifaulu mitihani ya uwakili na tarehe 20 Juni 2014 akatunukiwa kuwa Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania na mahakama zingine za chini isipokuwa mahakama ya mwanzo kwa namba ya uwakili 4220. Jebra Kambole amewahi kutajwa kama kijana wa wiki Tanzania na Gazeti la The Guardian mwaka 2014.


KUHUSIANA NA TAALUMA YAKE


Kwa sasa ni mmiliki mwenza wa kampuni ya sheria ya LAW GUARDS ADVOCATES iliyo na makao yake jijini Dar-es-Salaam Tanzania. Mbali ya kuendesha mashauri mahakamani amekuwa akitoa elimu ya sheria kwa umma wa watanzania kwa kuandika makala kwenye magazeti,kushiriki vipindi vya televisheni na redio na midahalo mbalimbali.https://www.youtube.com/watch?v=TaNGYOl3s_s Alijipatia umaarufu kwenye nyanja ya sheria nchini Tanzania , hasa baada ya kuanza kuwa wakili mtetezi katika kesi zenye kuvuta hisia za watanzania wengi mfano kesi dhidi ya wamiliki wa mtandao maarufu wa www.jamiiforums.com ambayo ilivuta hisia za wadau wengi wanaotetea uwepo wa uhuru wa kujieleza, pia kesi iliyoletwa https://en.wikipedia.org/wiki/Rebeca_Gyumi na taasisi yake ya Msichana initiative ili kupinga sheria ya ndoa za utotoni nchini Tanzania, Katika kesi hiyo Wakili Jebra Kambole na mteja wake https://en.wikipedia.org/wiki/Rebeca_Gyumi walishinda kesi hiyo.


NAFASI ZA UONGOZI


Mapema mwaka 2018 Jebra Kambole alichaguliwa na mkutano mkuu wa Chama cha Sheria Tanganyika (Tanganyika Law Society) uliofanyika kati ya tarehe 13 & 14 Aprili 2018 katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Mt. Meru jijini Arusha kuwa mjumbe wa Baraza la Uongozi la Chama hicho (Member of the Governing Council) na pia kuwa muwakilishi wa baraza hilo katika Kamati ya Katiba na mambo ya Sheria ya chama hicho.


Karibu![hariri chanzo]

Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na n) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Bwana Jerry tungefurahi sana kama unaweza kuamua kuchangia hapa. Hapa kuna makala ambayo bado ni fupi mno: http://sw.wikipedia.org/wiki/Jamii:Mbegu_za_sheria. Hapa ni orodha ya vichwa vya kisheria vinavyostahili kupata makala kwa Kiswahili http://meta.wikimedia.org/wiki/List_of_articles_every_Wikipedia_should_have/Expanded#Law.2C_68 Muhimukwetu si kutafsiri kila neno bali kufanya hitimisho inayoeleweka vizuri kwa wasomaji wetu. Unaonaje? Kipala (majadiliano) 21:22, 9 Juni 2014 (UTC)[jibu]