Majadiliano ya mtumiaji:Christian Anold Mosha

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na n) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

--Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:06, 29 Julai 2021 (UTC)[jibu]

Ndugu, unazidi kujaza Wikipedia yetu makala zisizoeleweka. Soma vizuri bango la hapo juu: ni marufuku kutumia tafsiri za kompyuta bila kuzisahihisha sana. Tafadhali. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:24, 9 Agosti 2021 (UTC)[jibu]
Ndugu, nakukumbusha tena kabla sijakuzuia. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:16, 9 Agosti 2021 (UTC)[jibu]

```:Habari, asante kwa kunikaribisha na kunirekebisha, ila nimeeshaacha kutumia tafsiri ya computer.Asante```

Kweli, umeanza upya. Endelea kujifunza kwa kuangalia tunavyosahihisha makala zako. Pia sijui kwa nini unapenda sana kuandika habari za mashoga na makahaba... Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:17, 10 Agosti 2021 (UTC)[jibu]
Habari Christian. Nimepitilia makala uliyoanzisha James Clifford (msanii). Hapa umemwaga google tr4anslate bila kuisahihisha.
Uliambiwa katika sanduku la kukukaribisha "NEVER post computer translated texts (like google-translate, mediawiki Content Translation etc.) nor copied texts/images from other webs to this site! ".
Ulipuuza utaratibu huu. Tunapata hasara kubwa kutokana na wachangiaji wanaoingiza matini zisizoeleweka, maana wanasababisha mzigo mkubwa wa kazi kwa wengine.
Nimekuzuia sasa. Uliwahi kupokea ombi na ushauri kutoleta google translate. Naomba niandikie kwenye ukurasa wangu majadiliano ya mtumiaji:Kipala kama uko tayari kusahihisha makala zako kabla ya kuendelea. Kipala (majadiliano) 10:33, 11 Agosti 2021 (UTC)[jibu]


Habari Kipala, samahani nipo tayari kusahihisha makala yangu kabla ya kuendelea--
Nimekurudisha kutokana na ahadi yako. Tafadhali angalia pia Dambudzo Marechera, sana Richard Wherrett (ni karibu ya kufutwa), Sharleen Spiteri (kahaba), Bernard Kabanda ("mzunguko wa muziki????", " baada ya onyesho lake katika Womad's Womad Reading ???" na mengine mengi). Kipala (majadiliano) 11:25, 12 Agosti 2021 (UTC)[jibu]

```sawa asante sana```

Taarifa ya zuio[hariri chanzo]

Taarifa ya kukuzuia!

Ndugu, imenibidi kukuzuia kwa sababu zinazotajwa chini. Wakati unapokuwa umezuiwa huwezi kuhariri isipokuwa penye huu ukurasa wako wa majadiliano. Unaweza kunijibu kwa kutumia “Email this user”.

Sababu ni kuwa umeingiza matini iliyopatikana kwa njia ya tafsiri ya kompyuta ikiwa na kasoro nzito ya lugha. Umearifiwa kwamba ni marufuku kumwaga matokeo ya google translate katika makala zetu. Wachangiaji wanaopuuza utaratibu huu wanasababisha hasara kubwa kwa Wikipedia yetu na kuwapa wengine kazi kubwa mno ya kusafisha makosa yao.

Bila shaka una nia nzuri kuchangia katika Wikipedia. Tutafurahi kushirikiana nawe lakini ni lazima ufuate utaratibu. Kazi yetu kama wakabidhi ni kulinda mradi huu.

Ukiwa tayari kufuata utaratibu pamoja na kupitia upya matini ulizozileta tayari, naomba uwasiliane nami kwa kufungua ukurasa wangu (bofya jina langu chini) na kuniandikia baruapepe kwa kubofya “Email this user” upande wa kushoto. Hapo nitaweza kukuruhusu tena. Hapo lazima uwezeshe njia kwa kufuata maelezo katika Wikipedia:Email.

Ndugu nimepitilia Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania. Umeendelea kutumia tafsiri ya kompyuta bila kusahihisha kwa kiwango cha kutosha. Naona kwamba umesahihisha mara kadhaa lakini kuna sehemu nyingi ambako tafsiri si sahihi au matini haina maana. Kipala (majadiliano) 10:45, 16 Agosti 2021 (UTC)[jibu]
Ninaongeza hapa {{Tanzania Mercantile Exchange]] ambayo haieleweki. Utahitaji kuitunga upya si kwa tafsiri ya neno kwa neno bali kwa kueleza kwa maneno yako mwenyewe kile kinachotokea huko. Soma Msaada:Tafsiri kabla ya kuanza. Ile kuhusu Tanzania min tiger plan nimependekeza ifutwe, maana lemma si sahihi, haina vyanzo (umekiangalia?) na haina maana kabisa - kwa nini unaleta makala kuhusu mipamgo iliyoanzishwa mwaka 2004 na kulenga 2020 kama huna habari matokeo yake ni nini kwenye mwaka 2021?Kipala (majadiliano) 13:14, 16 Agosti 2021 (UTC)[jibu]
Mengine unayohitaji kuangalia na kusafisha au kutunga upya ni Reli ya abiria ya Dar es Salaam, Dambudzo Marechera (bado makosa mazito na vigumu kuelewa); Richard Wherrett (mkurugenzi wa hatua?; hakuwa mshoga akiwa na miaka 17 bali alitambua alikuwa vile..; makala ya enwiki imefupishwa hadi kutoeleweka kwa nini iko kwenye wikipedia); Sharleen Spiteri (kahaba) (sentensi ya kwanza na vifungu vya "Ingawa kulikuwa ..." na vya mwisho bado havieleweki, makala inajaa makosa ya tahajia); Bandari ya Dar es Salaam (" Chama cha Kimataifa cha Bandari na Bandari" ???; viungo vya ndani ni hovyo sana maana hujaangalia kama makala ziko na tahajia ni namna gani kama vile Durban, sultani / usultani wa Zanzibar, Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki na kadhalika; nikisoma sentensi nakwama mara kwa mara), Upatikanaji wa mtandao nchini Tanzania ("viunganisho vya waya visivyo na waya ambapo milioni 1.2 na waya zilizokua na waya "????); Yetu Microfinance (uwezeshaji mdogomdogo  ???, fungu la Muhtasari); Kazi kwa watoto nchini Tanzania (vioungo vya ndani hovyo; fanya yote kwa maneno yako, si kwa kutafsiri); Mamlaka ya Mapato ya Tanzania. (lemma haina nukta; malaka si shirika....). Ndugu unaanzisha lemma kadhaa ambazo ni muhimu lakini huna uwezo wa kutafsiri. Kama unetumia maneno yake ingekuwa afadhali. Kipala (majadiliano) 14:15, 16 Agosti 2021 (UTC)[jibu]

Jina lako katika Makala[hariri chanzo]

Salamu, tazama katika makala zako ulizoanzisha hivi punde, makala zimekuwa zikitanguliwa na jina lako badala ya jina husika la makala, pia ni vyema kuunganisha makala yako na makala ya Kiingereza kabla ya kuendelea na makala nyingine,Amani sana Idd ninga (majadiliano) 21:38, 22 Februari 2022 (UTC)[jibu]

Salamu IDDI, makala zimetanguliwa na jina langu kwa kua bado ni draft, hivyo nikikamilisha nitaweka kaika jina husika la makala Ahsante Christian Anold Mosha (majadiliano) 22:04, 22 Februari 2022 (UTC)[jibu]