Majadiliano:Zohari

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Makala hii inasema, "Zohari ni sayari ya sita toka kwenye jua". Sayari ya sita ni "Saturn" kwa Kiingereza. Lakini Atlasi ya Kiswahili yangu kutoka Tanzania ina ramani ya sayari. Katika ramani hii Zohari ni sayari ya saba, na sayari ya sita ni "Sarateni". Sayari ya saba inaitwa "Uranus" kwa Kiingereza. Matt Crypto 11:40, 12 Februari 2006 (UTC)[jibu]

Majina ya sayari[hariri chanzo]

Kwa bahati mbaya sina atlasi ya Kiswahili nami; lakini nisingeshangaa kama kitabu cha shule kutoka Tanzania inaweza kuwa na kasoro hata makosa, nimeshaona makosa mbalimbali.

Nahisi ya kwamba "Zohari" ni sawa kwa ajili ya sayari ya sita kwa sababu zifuatazo:

  • majina ya sayari zilizojulikana tangu zamani yamepokelewa kutoka Kiarabu. Waarabu walijua sayari hadi Zohal = sayari ya sita. Sayari zisizoonekana haikuwezekana kupewa jina. Hivyo naona ni kosa katika atlasi ile kwani Zohari ni jina la Kiaarabu tena kwa sayari ya sita.
  • Kwa Kiarabu sayari ya sita ni "zohal";
  • kamusi zangu za Madan/Johnson zinataja Zohali kuwa "Saturn"
  • kijitabu cha Sebald "Maajabu ya ulimwengu" inataja Zohali kuwa sayari ya sita

Nitaweka makala ya "Mfumo wa jua na sayari zake" nikitaja majina kutokana na vitabu vyangu - halafu tuone. --Kipala 16:23, 12 Februari 2006 (UTC)[jibu]

Nyongeza[hariri chanzo]

Sayari za Uranus, Neptun na Pluto zimejulikana tu tangu kupatikana kwa darubini. Hiyo ndiyo sababu ya kwamba Wababiloni, Wagiriki na Waarabu wa Kale hawakujua sayari hizi wala kuwa na majina kwao. Sayari hizi zimeonekana na kupewa majina tangu darubini ilitumika huko Ulaya hivyo hata Waarabu hutumia majina haya kama "Uranus" n.k.

Vilevile naona haiwezekani ya kwamba jina kama "Zohari" imeweza kutaja sayari ya saba yaani Uranus kwa Kiswahili kwa sababu Waswahili wa kale hawakujua sayari hii. Lakini walijua sayari ya sita yaani Zohari na hawakuitaja kwa "Sarateni" neno ambalo ni "Pidgin" ya Kiingereza.--Kipala 22:15, 12 Februari 2006 (UTC)[jibu]