Majadiliano:Uislamu

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sijui je mistari hii inayofuata ina nafasi gani katika wikipedia? Hapo chini ni waraka inayojaribu kuonekana kama mkristo ameandika lakini ni wazi si ya kweli. Ni wazi kabisa waraka huu umeandikwa na mtu anayependa kulalamika kuhusu uhusiano kati ya madhahebu au dini mbalimbali huko Zanzibar. Lakini hasemi wazi anatumia uwongo. Wikipedia ni mahali pa elimu isitumike ovyo na vikundi vya kisiasa kupigania vita vyao! Tena hatii sahihi yake. Sijui wengine wanasemaje lakini mimi naona heri ifutwe! --Kipala 14:43, 25 Desemba 2005 (UTC)[jibu]

huu ni upumbavu haupaswi kuwepo hapa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mdau na mpenda maendeleo na amani!

Uislamu Zanzibar Inaelekea Wapi?[hariri chanzo]

Asalam aleykhum,

Hakika mada hii imenigusa mno na kunisikitisha sana kuona jnsi watanzania wenzetu wanavyotufanyia! Ila nina imani kubwa kuwa kwa nguvu zake Allah (SW) hakuna lolote watakalifanikiwa kwani njama za kuua uislamu katika sura ya dunia ilikuwepo tangia enzi za mitume wetu. Enzi za Bwana Mtume Muhammad (S.A. W) alipigwa vita sana lakini kwa uwezo wak Allah(SW) Mtume wetu Muhammad (SWA)alifanikiwa sana hadi sisi tumekuja kuikuta imani hii. Cha msingi nawaomba waislamu tushikamane kuuangusha utawala huu wa kidhalimu kwa amani katika kura za Oktoba na tuwe na msimamo thabiti. Mara Nyingi tunashindwa kwa kuwa hatuna imani thabiti kwa dini yetu. Tunapenda mno maisha ya hapa duniani badala ya kujitengenezea hatma kwa Mola wetu kesho tutakapokufa. Inafurahisha kuona kuwa wanatuhofia hivyo tushike uzi ule ule na sisi tuanzishe mashule na misikiti mikubwa tujenge vijijini. Mimi ni mtu wa bara (Tanzania Bara) ni Mwisilamu Mwanamke. Ningeomba waislamu kwa pamoja tujitahidi kujenga misikiti na vituo vya elimu kwa watoto na wakubwa ili tuwafufue watu kiimani. Suala si zito tu Zanzibar bali hata huku bara! Kinababa wakiislamu wanawaachia mabinti zao kuvaa hovyo kwa kufuaa tamaduni za kipuuzi za wakristo, hawawafundishi wake zao dini badala yake wanakwenda bar kulewa au kucheza bao! Jamani tuanzeni kuwa na misimamo kuanzia majumbani mwetu kila mtu akiwa na familia yenye msimamo hakika hawa makafiri hatatupata kwa misaada yao ya hospitali wala shule.

Wabillah Tawfiq

Mkereketwa - Bara

Kuondoa kopi-paste[hariri chanzo]

Nimeondoa mabadiliko hasa kutoka mtumiaji Niya ya saada aliyeingiza maudhui aliyokopi kwenye tovuti nyingine ambayo ni marufuku hapa wikipedia. (linganisha: majadiliano:saumu) Kipala (majadiliano) 14:12, 19 Septemba 2018 (UTC)[jibu]