Majadiliano:Silika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Makala haina JAMII hiusikanayo. Hivyo utabaki kuwa haipatikani katika fungu lake. Kingine: sijui silika kama neno la kitaalam au ni elimu ya jamii, kwani katika makala napata mchanganuo mwingi wa habari ulioambata na maelekezo ya kidi. Halafu, bado naona hamna INTERWIKI katika makala hii! Sasa, naomba nifahamishwe hii "SILIKA" ni kitu gani? Au kama makala ina uwezekano wa kuunganishwa kwa wiki zingine walau kidogo ningefahamu kilichosemwa ndani yake!--Mwanaharakati (Longa) 10:14, 1 Novemba 2008 (UTC)

Ndugu, neno silika nimelichukua kadiri ya Kamusi ya Kiswahili Sanifu likiwa na maana ya tabia ya kisaikolojia. Jamii husika inaweza kuwa Elimu jamii niliyoianzisha, lakini labda ni vizuri zaidi kuigawa na kuanzisha nyingine ya Elimunafsia. Kuhusu interwiki nimeshindwa kuiweka kwa sababu makala yangu ni ndefu na inahusika na makala mbalimbali za lugha nyingine. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:19, 1 Novemba 2008 (UTC)

Aha! Sasa wewe uoni hicho kivumbi kuandika makala ambayo katika wiki zingine si rahisi kuzielezea au ina mwingiliano na makala kadhaa zenye sawa na hizi (sana-sana za elimu ya jamii). Je, hii umetunga mwenyewe ama umesoma mahala fulani? Hebu tufahamishe hapo ni kipi kinachofanya makala nzuri kama hii ikose INTERWIKI?--Mwanaharakati (Longa) 10:29, 1 Novemba 2008 (UTC)
Ndugu, mtunzi wa makala hii ni mimi mwenyewe. Kama unaona inaleta kivumbi, tunaweza kuikata sehemusehemu:: --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:39, 1 Novemba 2008 (UTC)
Hapana, hapana. Nilitaka kujua kama makala hii ya kutafsri ama namna gani! Haya basi, je, waweza kulipeleka neno hili kwa lugha ya Kikwenu au Kiingereza angalau tupate maana nyingine itakayopelekea makala hii kuunganishwa katika Wikipedia zingine?--Mwanaharakati (Longa) 10:53, 1 Novemba 2008 (UTC)
Nimeshatafuta katika lugha mbalimbali (kama nilivyofanya kwa Uhuru wa nafsi) lakini nimeshindwa. Ndiyo sababu sikuweka interwiki. Sasa uamuzi kwenu, wakubwa!

Nje ya talk hii, labda umeona Babel imeleta tatizo upande wa Kihispania: nilijaribu kurekebishja leo, lakini nimeshindwa: inakubali template nikiweka 2, lakini si 1. Kuhusu picha nitajaribu siku nyingine. Asante sana. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:58, 1 Novemba 2008 (UTC)

Kwa upande wangu sina tatizo sujui Wazee wangu wanasemaje! Lakini naona iko sawa tu. Kuhusu Babel kwa Hispani katika msingi wa "A", nitakuuweka sawa hivi punde! Ahsante kwa maelezo yako.--Mwanaharakati (Longa) 11:33, 1 Novemba 2008 (UTC)