Majadiliano:Midomo

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mimi naelekea kuona mdomo ni sawa na mouth, si lips. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:15, 3 Januari 2021 (UTC)[jibu]

Ninapotafuta katika kamusi kadhaa, ninapata maoni kwamba maana asili ya mdomo ni lip. Kisha likapata maana ya mouth iliyofungwa. Mouth opening ni kinywa. Kwa Kikuyu, mouth ni kanua na lip ni mũromo. Kwa Kikamba, mouth ni kanywa na lip ni mulomo. Hata hivyo, naweza kuwa na makosa. ChriKo (majadiliano) 20:34, 3 Januari 2021 (UTC)[jibu]
Nimeongea sasa hivi na mwalimu mzuri wa Kiswahili. Katika isimu wanatumia "mdomo wa juu" na "mdomo wa chini" kuelezea fonolojia, lakini kwa matumizi mengi mdomo ni uwazi wa kupitishia chakula n.k. kama zinavyoonyesha kamusi mbalimbali. Ndiyo maana ya msemo "Ana mdomo mchafu". Lakini si dogma! Amani kwako na heri kwa mwaka mpya. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:38, 4 Januari 2021 (UTC)[jibu]
Sitajadili kile mwalimu huyu anachosema. Walakini, tayari kuna makala kuhusu "mouth". Inaitwa kinywa. Ili kudhoofisha wasiwasi wako, sasa napendekeza kubadilisha kichwa cha makala hii kuwa midomo. ChriKo (majadiliano) 14:06, 4 Januari 2021 (UTC)[jibu]