Majadiliano:Maundo

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kata ya Maundo[hariri chanzo]

Kata ya Maundo ni kata iliyopo Tarafa ya Namikupa katika wilaya ya Tandahimba, Mkoa wa Mtwara. Kata ina jumla ya vijiji 6 navyo ni Maundo, Kunandundu, Namahonga na Chiumo. Kata ina jumla ya watu 10232 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012. Kata ipo imepakana na msumbiji upande wa kusini pamoja na mto ruvuma ambao ni mpaka kati ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Msumbiji. Upande wa Magharibi imepakana na kata ya Mchichira na Kwanyama(Namikupa I). Kasikazini imepakana na kata ya Namikupa na kata ya Naputa. Upande wa mashariki kata ya Maundo imepakana na kata ya Chikongo.

Kata inajumla ya shule za msingi 6 na shule 1 ya sekondari ya Kata. Wastani ufaulu wa watoto kwa mwaka wa shule za msingi ni 82% na nafasi ya shule kiwilaya ni 1~10 na wastani wa ufaulu kwa shule ya sekondari ni 23%. Pia kata ina Zahanati moja na soko 4 ya bidhaa pamoja na maduka ya bidhaa wastani wa maduka 64 kiujumla.Kata ina jumla ya vyama vya ushirika 7 na maghara ya kuuzia mazao ya biashara mchanganyiko na Usafiri ni wa muda wote na hali ya hewa ni nzuri kwa wakati wote.

Shughuli kuu katika kata ya Maundo ni kilimo hususan kilimo cha Korosho, Muhogo, Viazi Vikuu, Mpunga, Mahindi, Kunde, Njugumawe, Mbogamboga, Ufuta, Ulezi na Uvuvi. Pia wananchi wa kata ya Maundo hujishughulisha na ufugaji wa Ng'ombe, Mbuzi, Kuku,Bata, Kanga na Njia. Zao kuu ambalo ni nyenzo kubwa ya kipato cha wananchi ni zao la Korosho kwa 75% na likifuatiwa zao la Muhogo kwa 13% ambalo pia hutumika kama zao la chakula. Wastani wa kipato cha mwananchi(per capital income) ni 300000~10000000+.

UTAMADUNI: Shughuli za kiutamaduni ni sherehe za ngoma ambazo huanza mnamo mwezi Disemba mpaka Januari. Shughuli kuu zinazofanyika katika kipindi hicho ni kuwafundisha vijana miongozo ya maisha pamoja na sherehe za kufunga mwaka kwa kumaliza mwaka wa zamani na kuanza mwaka mpya. Aidha wananchi wa Maundo ni wakarimu na wastaarabu wa hali ya juu

Makabila makuu yaliyopo kata ya maundo ni makonde, yao, sukuma, mwera, ngindo, chaga na waha.


                                                         KARIBUNI SANA MAUNDO.
                                                   Mr. Ahmadi Abdallah Ahmadi Chihipu