Majadiliano:Matamvua (samaki)

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Matamvua[hariri chanzo]

Mimi napendelea matamvua juu ya mashavu. Ikiwa maana ya mashavu ya samaki ni fish gills, basi fish cheeks ni nini kwa Kiswahili? ChriKo (majadiliano) 20:52, 1 Machi 2020 (UTC)[jibu]

Sikusikia (au sikumbuki) matamvua. Nikichungulia kamusi naona kweli ni visawe. Ila kwa majina yote mawili kuna tatizo yana maana mbalimbali. Mashavu ya samaki kwa kawaida ni "gills", lakini kuna pia watu wanaopenda kula nyama ya samaki inayopatikana kwenye shavu lake ("fish cheeks" sijui kama ni wengi wanaoijua). Upande mwingine Matamvua ya samaki ni "fishgills", ila "matamvua" yenyewe ni nyuzinyuzi za kitambaa kilichokatwa.
Tazama Kamusi ya Kiswahili Sanifu3: matamvua [matamvuwa/ nm (-) [ya-] 1 nyuzinyuzi zinazoachwa kama nakshi kwenye pindo la kitarnbaa k.v. kikoi. 2 nyuzi ambazo hazikusokotwa bali zimefumuliwa kidogo na kutiwa kasi: Nyuzi za ~. 3 nyuzinyuzi kwenye shavu la samaki ambazo huchuja hewa kutoka kwenye maji ili iingie mwilini mwa samaki. 4 nyuzinyuziza ufagio wa kupigia deki.
 ::Kwa hiyo tuhamishe Matamvua ya samaki? Kwangu sawa.

Kipala (majadiliano) 09:26, 2 Machi 2020 (UTC)[jibu]

Ni kweli, matamvua ni nyuzinyuzi fulani ("frills"). Na matamvua ya samaki ni nyuzinyuzi zake zilizopo kwenye "gills" zake na hakuna matamvua kwenye sehemu nyingine ya mwili wake. Kwa hivyo ninapendekeza ukurasa huu uhamishwe. ChriKo (majadiliano) 17:06, 2 Machi 2020 (UTC)[jibu]