Majadiliano:Mapenzi ya jinsia moja
Mandhari
ISTILAHI na tafsiri
[hariri chanzo]Aina kuu za wapenzi wa jinsia moja ni wasagaji, mashoga, wasenge na mabasha. Maneno hayo yanaweza kutumika kwa dhihaka au kwa lengo la kudhalilisha watu wa namna hiyo. Matumizi hayo yanaweza kuathiri vibaya hisia na heshima ya watu hao.
Nilipookozesha ni dhahiri mtoa mada hajui utamaduni wa Waswahili. Kama ametumia utamaduni wa Waafrika kwa lugha yao kuweka utamaduni wa Kizungu ni upotoshaji mkubwa. Waswahili hawawezi kusema MSENGE ama MFIRAJI mbele za watu. Ndiyo maana ili kupunguza ukali wa maneno, wataita SHOGA (MSENGE) na MFIRAJI (basha). Hiyo statement hapo juu inahitaji marekebisho makubwa kabisa. Visichanganywe. Said Mfaume (majadiliano) 08:27, 12 Desemba 2024 (UTC)
- Ndugu, aliyeweka maneno hayo ni Mmarekani mwenye asili ya Tanzania. Tuliwahi kuwasiliana naye kuhusu mada hizo tata, lakini mitazamo ni tofauti. Kwa jumla katika mradi huu wa kimataifa hatuwezi kupinga mno tabia hizo. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:13, 12 Desemba 2024 (UTC)
- Ikibidi hivyo hilo ni tatizo. Hata hivyo, makala ina mitazamo mingi sana ya kifalsafa na itikadi fulani badala ya tabia. Pengine ingepunguzwa baadhi ya mitazamo ili isiwe kubwa kiasi cha kwamba haina hata maana kuisoma. Isipishane sana na ENWIKI. Said Mfaume (majadiliano) 13:37, 12 Desemba 2024 (UTC)