Majadiliano:Magindu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Mabadiliko yanakuja magindu.[hariri chanzo]

Nakumbuka mbali xana nikifikilia waasisi wa kijiji chetu, mzee kisebengo, mzee makusi, mzee mazengo lufunga na wengineo wengi waliojitahidi kufikisha fikra za wazazi wetu wa sasa pale zilipo. Nakumbuka mbali sana nikiifikiria mama yangu akinipa shilingi mia nikanunue muhogo fungu moja kwa mzee mbega, nilikuwa na faraja xana na niliamini maisha yale yangeendelea mpaka sasa kumbe ndoto zangu zilikuwa ni sawa na kupaka rangi upepo. Wanafalsafa walisema hauwezi kutumia muda mrefu kulalamikia tatizo bali tumia akili ya ziada kutatua tatizo.

Magindu ni kijiji ambacho kina rasilimali nyingi ambazo kiuahalisia kama hamasa ikiwa kubwa na kila mwananchi akiwajibika kwa nafasi yake basi matatizo yatakuwa historia.

Ndugu zangu, napenda kutumia msemo wa mwalimu nyerere aliyewafananisha wasomi wanaosomeshwa ng'ambo na kulowea huko huko ni sawa na watu waliotumwa chakula mbali na kisha wasirudi nyumbani baada ya kupata chakula, kundi hilo la wasomi ni sawa na wauaji. Kwa kutumia hotuba hiyo nawahakikisha wana magindu kuwa NARUDI NYUMBANI.

narudi nyumbani kuhakikisha kwamba kunakuwa na heshima kwa utu wa wote, kunakuwa na usawa kwa makundi yote ya uzalishaji mali, watoto wetu wanapata elimu bora, huduma za afya zinapatikana bila matatizo, kufuatilia kwa karibu matibabu ya wajawazito na wazee, kuanzisha na kuboresha vikundi vya ujasiriamali, kusaidia upatikanaji ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda ili vijana wetu wapate ajira. Elimu ya uraia itatolewa kwa wananchi ili wazidi kutambua haki zao. Uongozi shirikishi kuanzia ngazi ya chini mpaka ya juu. Kuheshimu mamlaka zote kuanzia kitongoji mpaka ya kata. Vijana wetu wanapata fursa zaidi ya kuburudika kwa michezo ya aina tofauti.

NARUDI NYUMBANI, kuhakikisha kwamba kilimo kinakuwa cha tija na endelevu na kuhakikisha rasilimali za wanyonge zinarasimishwa ili kuweza kuwaletea tija . Nitakuwa mstari wa mbele kupaza sauti ili niwatetee wanyonge. Sit aogopa kusimamia haki kwa maslahi ya utu. Nitaheshimu utu na haki za binadamu.

Mungu Ibariki Magindu.

Erasto Makala. Bsc HIP.

LLLL