Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Madini ya bahari mfu

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nimeweka alama ya "FUTA" juu ya makala hii; naona ni makala ya kwanza ya mchangiaji mpya sitaki kumkatisha tamaa lakini hii haiwezi kubaki jinsi ilivyo. Florah ana nafasi ya kuisahihisha karibuni. Nataka kumsifu kwa sababu alijaribu tayari kufanya utafiti na kutafuta vyanzo.

  • A) Abadilishe lugha na kuandika kama makala ya kamusi. Hadi sasa alianza kama mchango wa majadiliano si makala ya maelezo. Atazame katika ukurasa wa Wikipedia:Mwongozo_(Anzisha_makala) na kurasa nyingine za mwongozo.
  • B) Achungulie makala zilizopo! Aliweka kiungo kwa makala ya Kiingereza Dead Sea, basi pale anaweza kuona upande wa kushoto chini kiungo kwa makala ya Kiswahili juu ya mada hiyohiyo. Iko tayari makala ya "Bahari ya Chumvi" ambalo ni jina lake la Kiswahili jinsi ilivyotumiwa tangu miaka mingi katika lugha za Biblia inapotaja ziwa hili. Kama "Bahari Mfu" imekuwa jina linaloeleweka, basi unaweza kuiongeza katika sentensi ya kwanza ya makala ya Bahari ya Chumvi.
  • C) Unaweza ama kuongeza habari za madini katika makala iliyopo AU kama unataka ktunga makala mpya unahitaji kutafuta habari za undani zaidi. Madini au Chumvi gani? Asilimia? Chanzo? Je ziko tayari tasnia zinazovuna / chimba madini haya? Yapi? Ni madini gani yanayoaminiwa kuchangia kwenye tiba?
  • D) Kama unahitaji ushauri ulizia tu! Utapata. Kipala (majadiliano) 23:16, 8 Januari 2018 (UTC)[jibu]