Majadiliano:Mshale (kundinyota)

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Naomba tusitumie jina la "Kausi" kwa ajili ya sayari ya Neptun.

  1. Kausi ni jina la "buruji ya falaki" (kwa lugha ya Waswahili asilia wenyewe) yaani kundinyota za zodiaki inayoitwa "sagittarius" kwa Kilatini/Kiingereza. Kwa hiyo ni jina linalojulikana kabisa katika utamaduni wa Waswahili lakini si kwa sayari. Ushuhuda wa kitaalamu uko hapa: J Knappert, fungu "In East Africa", makala AL-NUDJUM katika THE ENCYCLOPAEDIA OF ISLAM, LEIDEN BRILL 1997, VOLUME VIII NED — SAM, uk 105
  2. Ikiwa Neptuni ni sayari isiyoonekana kwa macho matupu ni sayari ambayo haikujilikana kwa tamaduni zote ya kale, pamoja na Waswahili na Kiarabu ambacho ni lugha ambako Waswahili walipokea majina mengi ya nyota. Hivyo pia "Kausi" kutoka kwa Kiarabu القوس al-qaus inayomaanisha upinde yaani zodiaki inayoitwa sagittarius katika nchi za magharibi .
  3. Mtaalamu wa lugha za Kiafrika Jan Knappert aliyekusanya majina ya nyota na sayari kwa Kiswahili mnamo miaka ya uhuru wa Tanzania na Kenya aliandika "Swahili astrologers concentrate first and foremost on the signs of the Zodiac, Buruji za Falaki, whose names are all from Arabic: Hamali, Aries - Mizani, Libra - Thauri, Taurus - Akarabu, Scorpio - Jauza, Gemini - Kausi, Sagittarius - Saratani, Cancer - Jadi, Capricornis - Asadi, Leo - Dalu, Aquarius - Sumbula, Virgo - Hutu, Pisces ... The Swahili names of the Planets are: Mercury, Utaridi; Venus, Zuhura; Mars, Mirihi; Jupiter, Mushitari; and Saturn, Zohali." (ling. chanzo hapo juu)
  4. Nahofia kweli ya kwamba wakati wa kutunga kamusi ya KAST makosa kadhaa yaliingizwa katika majina ya sayari na kwa bahati mbaya yalinakiliwa na kamati zilizotunga muhtasari ya sayansi kwa shule ya msingi. Nimependekeza tutaje matumizi yaliyo tofauti kama yaliingia katika vitabu lakini tusitumie kama lemma dhidi ya ushahidi wa kitaalamu. Kausi, Sumbula na Sarateni ni zote majina ya kundinyota yaliyojulikana kwa mabaharia na wanafalaki wa Afrika ya MAshariki tangu karne nyingi na ushuhuda wake upo. Si Knappert (aliyetunga orodha kubwa ya majina ya nyota) peke yake nimepata pia uthebitisho wa Profesa Sengo wa Chuo Kikuu Huria Dar kuhusu majina ya sayari. Kipala (majadiliano) 22:52, 17 Februari 2017 (UTC)[jibu]