Majadiliano:Kamusi

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kamusi ni kitabu cha marejeo chenye msamiati uliokusanywa kutoka kwa wazungumzaji wa jamii fulani na kupangwa kwa utaratibu maalumu kisha kufafanuliwa kwa namna ambayo msomaji aweze kuelewa.

   ====Muundo wa kamusi====

Kimuundo kamusi imegawanyika katika sehemu kuu tatu

  • 1.Utangulizi wa kamusi
  • 2.Matini ya kamusi
  • 3.Sherehe ya kamusi
   ====1.Utangulizi wa kamusi====

Hii ni sehemu ya kwanza ya kamusi,sehemu hii hujumuisha muhtasari wa sarufi ya lugha yenyewe pamoja na maelezo ya namna ya kutumia kamusi.

   ====2.Matini ya kamusi====

Hii ni sehemu yenye vidahizo vyote vya kamusi husika,kuanzia alfabeti a-z vidahizo vyote huolozeshwa hapa na kufafanuliwa.

   ====3.Sherehe ya kamusi====

Ni taarifa zinazoingia mwishoni mwa kamusi.

   ====Aina za kamusi====

Kuna aina tatu za kamusi ambazo ni

  • 1.Kamusi wahidia
  • 2.Kamusi thaniya
  • 3.Kamusi mahuluti
   1.Kamusi wahidia

Ni aina ya kamusi inayoandikwa kwa lugha moja.kamusi hii huwalenga wazungumzaji wa lugha hiyo na wakati mwingine kama wanajifunza lugha ya pili au lugha ya kigeni.

   2.Kamusi thaniya

Ni aina ya kamusi iliyoandikwa kwa lugha mbili.Vidahizo huandikwa ka lugha moja na maelezo ya maana ambayo aghalabu huwa ni visawe huandikwa kwa lugha nyingine.

   3.Kamusi mahuluti

Ni aina ya kamusi iliyoandikwa kwa lugha zaidi ya mbili.Vidahizo vya kamusi mahuluti hupatiwa vusawe katika lugha mbili au zaidi.

   Umuhimu wa kamusi
  • 1.hueleza maana ya maneno
  • 2.huonyesha asili ya neno
  • 3.husaidia mtu kujifunza lugha ya kigeni
  • 4.hubainisha kategoria
  • 5.huongeza maarifa zaidi kuhusu lugha ya wazungumzaji