Majadiliano:Haki ya kuishi

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Majadiliano:Haki ya Kuishi)

Haki ya kibinadamu au ya kila kiumbe?[hariri chanzo]

Naona lugha "kila kiumbe" ni gumu kidogo. "Kila kiumbe" ni pamoja na wadudu, inzi, samaki, kama ninaelewa Kiswahili sawa. Sina uhakika kwa nini waliandika "being" badala ya "human" katika makala ya Kiingereza. Ni kweli kuna wanafalsafa kama Peter Singer wanaona kimsingi hakuna tofauti ya kimsingi baina ya binadamu na wanyama wengi, ziko pia dini kama Ujain ambazo zingeingiza kila uhai katika amri zao, lakini kwa jumla ni msimamo wa wachache nisipokosei. Ni verma kuwataja, lakini sidhani inafaa sana katika ufafanuzi wa kimsingi kwa sababu inajadiliwa hasa mbele ya mandharinyuma ya haki za binadamu, sivyo? Kipala (majadiliano) 15:30, 2 Juni 2021 (UTC)[jibu]

Makala inaeleza haki ya kuishi ya ki binadamu, je jina libadilike?BrixL (majadiliano)
Kutokana na ufafanuzi mwanzoni makala ilielekea zaidi upande wa viumbe vyote (hoja ambalo lipo); jinsi inavyokaa mwanzoni sasa hakuna tatizo tena. Kipala (majadiliano) 18:26, 2 Juni 2021 (UTC)[jibu]