Majadiliano:Kodivaa
Weka madaMandhari
(Elekezwa kutoka Majadiliano:Cote D'Ivoire)
Latest comment: miezi 11 iliyopita by Kisare in topic Ivory Coast, Cote d'Ivoire, na Kodivaa
Ivory Coast, Cote d'Ivoire, na Kodivaa
[hariri chanzo]@Muddyb Naona umehamisha makala hii kwenye "Ivory Coast". Lakini ivory coast ni jina lake katika Kiingereza. Jina sanifu katika Kiswahili kwa mujibu wa TUKI ni "Kodivaa". Hata Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa, na serikali ya Tanzania zinataja "Kodivaa". Tufuate TUKI na tuweke "Kodivaa" kama jina kuu la makala kwa sababu ya kuwa jina sanifu, na vilevile tunaweza kutaja Cote d'Ivoire na Ivory Coast katika sentensi ya kwanza ya makala, kwa sababu ya kuwa majina yanayotumiwa mara nyingi pia. Unaonaje? Kisare (majadiliano) 20:18, 11 Januari 2025 (UTC)
- Niliona pia katika kamusi yangu ya Kiswahili - Kiswahili (2013) inataja Kodivaa. Siku nyingi sikuchukua hatua kwa sababu tunafuata sana media zetu. Unaweza kuhamisha kwenda Kodivaa. Sawa tu. Hata nchi nyingi. Itapendeza kama tukiweka na marejeo ya majina pale mwanzoni ili isionekane tumejitungia. Ukiwa una toleo la TUKI pia unaweza kulitaja kama rejea. MuddybLonga 07:44, 16 Januari 2025 (UTC)
- Sikuona jibu yako hadi sasa hivi, samahani. Nitaihamisha na kutaja rejeo kutoka TUKI. Pia Nitataja majina mengine kama cote divoire, ivory coast, n.k. katika sentensi ya kwanza. Kisare (majadiliano) 19:40, 14 Februari 2025 (UTC)