Majadiliano:Chinua Achebe

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Muhtasari Riwaya hii inamhusu shujaa Okwonko ambaye kwa kufanya kazi kwake kwa bidii anakuwa miongoni mwa wakwasi wa Kijiji cha Umuofia na kupewa nafasi miongoni mwa waheshimiwa wa jamii.Babayake mzee Unoka alikuwa amezoea tabia ya kulaza damu ndio maana kaishia kuishi madongo poromoka na hakupewa cheo chochote na kijiji chake licha ya kutoka kwenye kijiji cha mashujaa yeye alikuwa tu shujaa wa ulumbi na kupiga nzumari.

 Okwonko ni kinyume cha babake na hakupenda kuwa mvivu ndiposa akaamua kuuasi umaskini kwa kufanya kazi kwa bidii na kujilimbikizia sifa nyingi kama mwanamume asiye na woga na asiye penda mzaha.Tabia hii ya Okwonko inamfanya kuchukia chochote kile alichokipenda babaye.
  Katika umri wa miaka kumi na saba Okwonko alikuwa na Ghala kubwa la viazi vikuu na wake watatu,alikuwa kashaoneka kifaranga ambaye bila shaka angekuwa jogoo wa kuheshimiwa na kuku wote.Pia alikuwa mwana miereka hodari sana na alimwangusha shujaa alipewa lakabu ya paka kwa sababu mgongo wake haukuwa umebwagwa chini.
  siku kukatoekea mkosi kwa kijiji cha Umofia ambao ulitekelezwa na kijiji jirani,basi ili kuepuka vita basi ikabidi kijana aitwaye Ikemefuma atolewe ili keupusha vita kulingana na matakwa ya mizimu.Kijana huyu anapelwa kuishi na jammaa ya okwonko huku wakisubiri hatma yake.Ikemefuma anamvutia Okwonko na kupendana sana na mwanaye Nwoye.Baadaye mizimu inaamua kuwa auwae lakinini onuo linatolewa na wazee kuwa Okwonko asishiriki katika mauaji yake ,lakini Okwonko kwa kuogopa kuitwa muoga anmuua kijana huyu.Huu ndio mwanzo wa masaibu ya Okwonko.
  Akiwa kwenye mazishi bunduki yake inafyatuka ghafla nakumuua kijana wa marehemu,Hukumu inatolewa kulingna na mila na desturi na inambidi Okwonko aende uhamisho kwa wajomba wake kwa muda fulani.
Kipindi chake cha kukaa uhamishoni kinapoisha anarudi na kukuta kwamba Umuofia imepoteza umaarufu na ushujaa wake mila na desturi ziko katika hali ya kuangamia kutokana na kuenuea kwa ukristo na pia kuwepo kwa kwa serikali ya kiingereza.
  Okwonko anamuua kuwa lazima wakristo wamalizwe kwa kutokana na tabia yao ya kuzikeli mila za kiafrika na hata miungu na mizimu ya Umofia .Mkriso mmoja anamvua gwanda mzimu mmoja na kuwagadhabisa wanakijiji ambao wanalibomoa kanisa. Hatua hii inaigagadhabisha serikali ambayo inawatia nguvuni Okwonko na wenzake,kijiji kinashikwa na kiwewe kwa kuwa mtu mweupe hakuwa na huruma kkwani wakikuwa nbado hawajasahau kile alichofanya kule Abame ambao walikuwa wamejaribu kuasi utawala wa kizungu.

Hatimaye baada ya kuachiliwa Okwonko nashindwa kustahili na kujitia kitanzi kwani yeye hangeweza kuishi huku akiona kuwa kijiji chao kilikuwa kimepoteza umaaruru na hakuna mashujaa waliokuwa wamesalia.

MANDHARI Hadithi hii imesimuliwa kutoka mazingira ya mashambani ambako watu walikuwa bado hawaja staarabishwa na walikuwa na mila itikaji baadhi yazo zilikuwa mbaya sa kama kuwaua mapacha kwa kuatupa msitunni na pia kuwatenga watu waliojulikana kama onsu pamoja na vizazi vyao na haawakuruhusiwa kunyoa nywele zao.