Majadiliano:Azimio la Kimataifa juu ya Haki za Binadamu

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jina la makala[hariri chanzo]

Tovuti rasmi ya UM inatumia lugha ya "Taarifa ya ulimwengu juu ya haki za binadamu" (tazama tovuti inayotajwa kwenye makala yenyewe); kama mwandishi wa kwanza wa makala hii nina wasiwasi juu ya lugha hii. Naomba Waswahili wachangie kama lugha ya tafsiri ya UM inaeleweka. KAma ndiyo basi tuhamishe huko na kusahihisha makala. --Kipala (majadiliano) 19:50, 23 Mei 2008 (UTC)[jibu]

Labda kuwe na kuelekezea pia kwa: Tangazo la Ulimwengu la Haki za Binadamu. Au Tangazo Kiulimwengu la Haki za Binadamu. Hapo vipi?--Mwanaharakati (majadiliano) 05:28, 24 Mei 2008 (UTC)[jibu]
Swali langu la kwanza: Je "Taarifa ya Ulimwengu" inaeleweka au la? --Kipala (majadiliano) 07:24, 24 Mei 2008 (UTC)[jibu]
Ni sawa tu. Inaeleweka.--Mwanaharakati (majadiliano) 07:44, 24 Mei 2008 (UTC)[jibu]
Vipi kuhusu: Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu? Ni wazo tu!--MwanaharakatiLonga 15:26, 14 Machi 2012 (UTC)[jibu]
Bingo! naona inaeleweka zaidi. Tena nimeangalia upya ukurasa wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora; hapo kwenye "Documents" iko sasa AZIMIO LA ULIMWENGU JUU YA HAKI ZA BINADAMU. Kipala (majadiliano) 17:40, 14 Machi 2012 (UTC)[jibu]
Eh, kweli umechimba! Sasa chagua... Naona hata lile la Utawala Bora linafaa kabisa. Tuendelee!!! Wako, Muddyb au,--MwanaharakatiLonga 12:41, 24 Machi 2012 (UTC)[jibu]