Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Maisha Yangu Baada ya Miaka Hamsini ni kitabu kilichoandikwa na Shaaban Robert mwenyewe akielezea historia na matukio yaliyotokea katika maisha yake na changamoto mbalimbali alizozipitia katika maisha yake ya kikazi kama muajiriwa wa Serikali na baadae kama muandishi wa mashairi.

Kitabu hiki kitawasaidia sana wasomi, wataalamu na waandishi wa fasihi ya Kiswahili katika kufanya utafiti wa masuala mbalimbali yanayohusu fasihi kwa ujumla na wanafasihi wake. [1]

Ndani ya kitabu hiki zinapatikana zile tenzi mbili maarufu za Utenzi wa Hati na Adili ambazo aliwaandikia watoto wake wawili Mwanjaa na Suleyman [2]

Japokuwa ametumia lugha ya kifasihi sana katika kitabu hiki, lakini Shaaban Robert ameweza kueleza mambo mbalimbali aliyowahi yapitia kama vile ubaguzi wa rangi aliowahi fanyiwa wakati anasafiri kikazi ndani ya Tanganyika wakati wa ukoloni tukio ambalo lilitokea 13 Julai 1944 wakati anatoka Korogwe, mkoa wa Tanga, kuelekea Mpwapwa.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "UCHAMBUZI WA KITABU CHA MAISHA YANGU NA BAADA YA MIAKA HAMSINI-MWANDISHI: SHAABAN ROBERT – Mwalimu Wa Kiswahili" (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2020-02-07. [dead link]
  2. Robert, Shaaban, 1909-1962. (1991). Maisha yangu : na, Baada ya miaka hamsini (toleo la New ed). Dar es Salaam: Mkuki na Nyota. ISBN 9976-973-16-0. OCLC 34708545. 
Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.