Nenda kwa yaliyomo

Mai Bhago

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mai Bhago anayejulikana pia kama Mata Bhag Kaur, alikuwa mwanamke wa dini ya Sikh aliyeongoza wanajeshi wa Sikh dhidi ya Mughals mwaka 1705. Alikuwa mpiganaji stadi sana vitani na anaheshimiwa kama mtakatifu-shujaa katika dini ya Sikh. Anajulikana kwa kuhamasisha Wasikh 40 (Chali Mukte) waliokuwa wamemwacha kiongozi wa dini ya usikh Guru Gobind Singh wakati wa kuzingirwa kwa mji mtakatifu wa Wasikh wa Anandpur Sahib na kuwarudisha vitani.

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]
Nyumba ya ibada ya Usikh ya Mai Bhango

Mai Bhago alizaliwa katika familia ya Jat,[1] katika kijiji cha mababu zao cha Chabhal Kalan, katika Jhabal Kalan, wilaya ya sasa ya Tarn Taran katika eneo la Punjab nchini India.[2] Alilelewa katika familia ya Sikh iliyojitolea sana kwa imani. Baba yake, Malo Shah, alikuwa amejiunga na jeshi la Guru Hargobind[3] na kama baba yake, Mai Bhago pia alijifunza Shaster vidya (mafunzo ya silaha). Alikuwa mjukuu wa Bhai Pero Shah, ndugu mdogo wa Bhai Langah, kiongozi wa vijiji 84 aliyesilimu na kuingia katika dini ya Sikhism wakati wa Guru Arjan Dev (1563–1606), Guru wa tano wa Sikh.[4] Alikuwa na kaka wawili, Dilbagh Singh na Bhag Singh.[5] Akiwa msichana mdogo, wazazi wake walimpeleka katika mji wa Anandpur Sahib kupata darshan ya Guru Gobind Singh ambayo hutazama kwa heshimamtu mtakatifu,sanamu au kitu kitakatifu kwa heshima ya kiroho. Aliolewa na Bhai Nidhan Singh wa Patti.[6]

Mapambano dhidi ya Wamughal

[hariri | hariri chanzo]

Katika jaribio la kumkamata Guru, jeshi kubwa la Mughal likiongozwa na Wazir Khan wa Sirhind chini ya amri ya Mfalme Aurangzeb lilielekea mji wa Anandpur Sahib pamoja na majeshi ya Mughal kutoka Lahore na Kashmir.[7]

Kuondoka kwa Chali Mukte (Wasikh 40 “waliokombolewa”)

[hariri | hariri chanzo]

Karibu mwaka 1704[8] wakuu wa vilima walioungana na Mughal waliizingira mji wa Anandpur Sahib na kudai iachwe, wakikata mahitaji ya chakula kwa miezi kadhaa.[9] Walitangaza kwamba Sikh yeyote atakayesema “si Sikh wa Guru Gobind tena” angeachwa salama, vinginevyo angeuawa. Kundi la Wasikh 40 (Chali Mukte),[10] wakiongozwa na Mahan Singh Rataul, walimwambia Guru Gobind Singh kwamba hawakuwa tena Wasikh wake. Guru aliwaambia waandike hati ikisema “Sisi si Wasikh wako tena” na wasaini. Wote arobaini (isipokuwa mmoja) walitia saini na kuondoka.

Jibu la Mai Bhago

[hariri | hariri chanzo]

Mai Bhago alihuzunika kusikia kwamba baadhi ya Wasikh wa eneo lake waliokwenda kupigana kwa niaba ya Guru walikuwa wamemwacha katika hali ngumu. Aliwakosoa hadharani, na kwa aibu ya kitendo chao waliamua kurejea. Mai Bhago aliwahamasisha na kuandamana nao kumtafuta Guru aliyekuwa akisafiri katika eneo la Malwa.

Matukio yaliyofuata katika mji wa Anandpur Sahib

[hariri | hariri chanzo]
Kuondoka kwa Guru kutoka ngome
[hariri | hariri chanzo]

Mjumbe alifika na kiapo kilichosainiwa na mfalme wa nasaba ya Wamughal, Aurangzeb juu ya Qurani, akimhakikishia Guru kwamba akitoka ngomeni, amani ya kudumu itapatikana. Guru hakuviamini viapo hivyo,[11] lakini aliamua kuondoka ili kufichua unafiki wa Wamughal.

Kutengana kwa familia ya Guru
[hariri | hariri chanzo]

Guru Gobind Singh aliondoka mji wa Anandpur. Watoto wake walitenganishwa katika vurugu za kuondoka. Wadogo wawili, Sahibzada Zorawar Singh na Sahibzada Fateh Singh, waliandamana na bibi yao Mata Gujari Kaur, huku wakubwa wawili, Sahibzada Ajit Singh na Sahibzada Jhujhar Singh, wakiwa na baba yao. Katika vita iliyoitwa battle of Chamkaur, wanawe wakubwa waliuawa kishujaa. Guru aliondoka katika kijiji cha Chamkaur kwa amri ya Panj Pyare.

Vita vya Muktsar huko Khidrana

[hariri | hariri chanzo]
Uchoraji unaomuonyesha Mai Bhago katika Vita vya Muktsar
Makala kuu: Battle of Muktsar

Guru alikuwa amefika kijiji cha Khidrana wakati Mai Bhago na wenzake walipomfikia. Eneo hilo lilikuwa na bwawa pekee la maji ambalo pia lilikuwa limetekwa na jeshi la Mughal lililokuwa likimfuatilia Guru.

Mai Bhago na wenzake walishambulia jeshi la Mughal lililokuwa na askari wapatao 10,000. Mwishowe waliwalazimisha kurudi nyuma huku majeshi ya Guru yakirusha mishale kutoka vilimani karibu. Guru alipofika uwanjani, aliwakuta wote wameuawa isipokuwa Mai Bhago na Mahan Singh. Mahan Singh alifariki mikononi mwa Guru. Wasikh wote arobaini walifia hapo pamoja na kaka na mume wa Mai Bhago na wakapata hadhi ya mashahidi (martyrdom).

Guru Gobind Singh aliwabariki arobaini hao kama Chali Mukte – Arobaini Waliokombolewa. Mai Bhago aliyekuwa amejeruhiwa vibaya alichukuliwa chini ya uangalizi wake.

Kuishi na Guru

[hariri | hariri chanzo]

Mai Bhago aliishi na Guru Gobind Singh huko Talwandi Sabo. Huenda alivaa mavazi ya Nihang. Guru alipokwenda kituo kitakatifu cha Usikh cha Hazur Sahib, Mai Bhago alikuwa mmoja wa walinzi wake kumi, akiwa amevaa mavazi ya kiume na kujihami kwa mkuki mkubwa na bunduki.

Mai Bhag Kaur huko Janwada

[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kifo cha Guru Gobind Singh huko Nanded mwaka 1708, Mai Bhag Kaur alihamia kusini zaidi na kuishi katika kijiji cha Janwada, kilomita 11 kutoka Bidar katika Karnataka. Alianzisha makazi yake ya kiroho na kujitolea katika tafakari na kufundisha Gurmat(mwongozo wa Guru). Makazi yake sasa ni mahali pa ibada panapojulikana kama Gurdwara Tap Asthan Mai Bhago ambayo ni nyumba ya ibada ya Usikh.

Uchoraji wa karne ya 20 wa Mai Bhago

Mwaka 1788, Mohan Singh, Jathedar wa Hazur Sahib, alijenga mnara(Bunga) kwa kumbukumbu yake. Silaha za Mai Bhago zimehifadhiwa katika eneo la Hazur Sahib huko Nanded, India. Kazi za sanaa za kisasa mara nyingi humwonyesha akiwa amevaa kilemba vitani. Amekuwa mfano bora wa mwanamke wa Sikh na ishara ya ujasiri kwa wanawake wa Sikh.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Thornton, S. A. (2008). "BHAGO, MAI". Katika Smith, Bonnie G. (mhr.). The Oxford Encyclopedia of Women in World History. Juz. la 1. Oxford University Press. uk. 226. ISBN 978-0-19-514890-9.
  2. "Search Gurbani : Gurbani Research Website". Iliwekwa mnamo 2022-05-22.
  3. Smith, Bonnie (2008). The Oxford encyclopedia of Women in World History, Volume 4. Oxford University Press. uk. 226. ISBN 9780195148909.
  4. Dalbir Singh Dhillon (1988). Sikhism Origin and Development. Atlantic Publishers & Distributors. uk. 152.
  5. Nihang, Nidar; Singh, Parmjit (2008). In the Master's Presence: the Sikh's of Hazoor Sahib. London: Kashi House. uk. 54. ISBN 9780956016829.
  6. Arneja, Simran (2009). Ik Onkar One God. Simran Kaur Arneja. uk. 102. ISBN 9788184650938.
  7. Shaw, Jeffrey; Demy, Timothy (2017). War and Religion: an Encyclopedia of Faith and Conflict. ABC-CLIO. uk. 576. ISBN 9781610695176.
  8. Fenech, Louis (2013). The Sikh Zafar-namah of Guru Gobind Singh. New York: Oxford University Press. uk. 18. ISBN 9780199931453.
  9. Singh, Teja; Jaggi, Rattan (1988). Essays in Sikhism. Languages Department Punjab. uk. 57.
  10. Singh, Harbans (2005). The Encyclopedia of Sikhism. New Delhi: Hemkunt Press. uk. 42. ISBN 9788170103011.
  11. Anand, T K (2005). Essence of Sikhism – 7. New Delhi: Vikas Publishing House. uk. 37. ISBN 9788125919483.