Mabel Balfour
Mabel Balfour alikuwa mwanaharakati wa vyama vya wafanyakazi kutoka Afrika Kusini na mpinga ubaguzi wa rangi (apartheid).
Mwanzoni alijihusisha na vyama vya wafanyakazi wa sekta ya chakula na makopo. Baada ya viongozi wengi wa South African Congress of Trade Unions (SACTU) kukamatwa katika Kesi za Uhaini za mwaka 1956, alijiunga na Kamati ya Uongozi mwaka 1957.[1]
Balfour alijulikana kwa uwezo wake wa kuwapa wafanyakazi moyo katika nyakati ngumu.
Mwaka 1958 alikamatwa kutokana na kushiriki katika maandamano ya “April Stay-At-Home” na kuhukumiwa kulipa faini ya pauni 20 au kufanya kazi ngumu kwa siku 30 kwa kosa la kuwachochea wafanyakazi wasio wazungu katika eneo la Rand. Hata hivyo, adhabu hiyo ilisimamishwa.
Mwaka 1962 alikua Katibu Mkuu wa African Food and Canning Workers Union (A-FCWU) katika Transvaal.
Mwaka 1963[2] alipigwa marufuku kisiasa na kuwekwa chini ya kifungo cha nyumbani mjini Roodepoort.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Mabel Balfour". v1.sahistory.org.za. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-10-05. Iliwekwa mnamo 2026-05-23.
- ↑ Berger, Iris (1992). Threads of Solidarity: Women in South African Industry, 1900-1980 (kwa Kiingereza). Indiana University Press. ISBN 978-0-85255-078-6.
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mabel Balfour kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |