Ziwa Michigan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
SS Badger ikifanya safari kati ya Manitowoc na Ludington
Ziwa Michigan pamoja na maziwa makubwa
Chicago

Ziwa Michigan ni moja kati ya maziwa makubwa ya Amerika ya Kaskazini kwenye sehemu ya Marekani pekee.

Ziwa Michigan limepakana na majimbo zifuatazo: Michigan, Indiana, Illinois na Wisconsin. Michigan na Wisconsin zinatawala sehemu kubwa ya ziwa.

Ziwa Michigan hupokea maji yake kutoka kwa mito mingi inayoisha humo; maji yake hutoka kwenda Ziwa Huron kupitia Straights of Mackinac. Majiji mawili makuu ni Chicago na Milwaukee.

Vipimo[hariri | hariri chanzo]

Ziwa lina urefu wa kilomita 494 na upana mkubwa wa 190 km. Uso wake una eneo la 58,000 km2. Kina cha wastani ni 85 m lakini kina kikubwa chafikia 281 m.

Maziwa Makubwa[hariri | hariri chanzo]


Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ziwa Michigan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.