Yohane Baptista de La Salle

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha rasmi ya Yohane Baptista de La Salle ilivyochorwa na Pierre Leger.
Sanamu yake katika kanisa la Jean-Baptiste de La Salle, Paris.
Masalia yake katika makao makuu ya shirika mjini Roma, Italia.

Yohane Baptista de la Salle (kwa Kifaransa: Jean-Baptiste de La Salle; Reims, Ufaransa, 30 Aprili 1651 - Saint-Yon, Rouen, Ufaransa, 7 Aprili 1719) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mlezi wa vijana wengi, hasa fukara, ambaye kwa ajili ya malezi yao ya kiutu na ya Kikristo alianzisha pia kwa tabu nyingi shirika la Mabradha wa Shule za Kikristo. Anahesabiwa mwanzilishi wa shule Katoliki duniani. De La Salle anahesabiwa pia kuwa wa kwanza kuendesha chuo cha ualimu (1685).

Anaheshimiwa kama mtakatifu na msimamizi wa walimu.

Sikukuu inaadhimishwa kila tarehe 7 Aprili[1] au 15 Mei.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Akifuata njia ya upadri tangu utotoni, alimaliza masomo na kupata upadirisho tarehe 9 Aprili 1678.

Miaka miwili baadaye alipata udaktari wa teolojia.

De La Salle aliingia kazi ya malezi taratibu, bila ya kukusudia, kadiri ya matukio na watu aliokutana nao.

Juhudi zake za kuanzisha shirika la mabradha tu kwa ajili ya kuendesha shule zilipata upinzani mkubwa kwa sababu ulikuwa mpango mpya.

Pia mbinu zake zilikuwa hazijazoeleka, kama vile kutumia lugha ya kawaida na kutodai ada yoyote.

Hata hivyo alifaulu kuanzisha mtandao wa shule nchini Ufaransa.

Heshima baada ya kifo[hariri | hariri chanzo]

Alitangazwa na Papa Leo XIII kuwa mwenye heri tarehe 19 Februari 1888 na mtakatifu tarehe 24 Mei 1900.

Papa Pius XII alimtangaza msimamizi wa walimu wote tarehe 15 Mei 1950.

Athari yake[hariri | hariri chanzo]

Kazi yake ilienea haraka. Leo duniani shirika lake lina mabradha 3,000 (mbali ya walei na watawa 75,000 wanaoshiriki kazi yao) wanaolea vijana kama 900,000 katika vituo vya malezi 1,100 vya nchi 80.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.