Yael Abecassis

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Yael Abecassis
Alizaliwa 19 Julai 1967 (1967-07-19) (umri 56)
Ashkelon, Israel
Kazi yake Mwigizaji
Mwanamitindo
Ndoa Lior Miller (1996–2003)
Roni Duek (2005–)

Yael Abecassis (Hebrew: יעל אבקסיס‎ ‎; amezaliwa Ashkelon, Israel, 19 Julai 1967) ni mwigizaji filamu na mwanamitindo kutoka nchini Israel.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Yael Abecassis alizaliwa na Wayahudi kutoka Moroko. Ni binti Raymonde Abecassis, mwigizaji na mwimbaji wa Israel.[1]

Abecassis alioana na mwigizaji wa Israel Lior Miller mwaka 1996 na kujaliwa mtoto mmoja. Walitalakiana mwaka 2003. Kwa sasa ameolewa na mjasiriamali Ronny Douek.

Kazi ya uigizaji na mitindo[hariri | hariri chanzo]

Yael Abecassis alianza uanamitindo akiwa na umri wa miaka 14. Baadae alijikita katika runinga na filamu, akionekana katika matangazo na kuwa mhusika mkuu aliyetambulika kwa jina la Rivka katika filamu ya Kadosh. Ni filamu ya mwaka 1999 ikiongzwa na Amos Gitai. Katika miaka ya tisini, alikuwa mtayarishaji wa vipindi vya watoto katika runinga ya Israel na kutayarisha video za muziki kwa watoto. Mwishoni mwa miaka ya 1990, aliacha kazi ya runinga na kujihusisha na uigizaji.

Filamu alizoigiza[hariri | hariri chanzo]

  • Hunting Elephants (2013), Dorit
  • Prisoners of War (2010), Talia Klein
  • Shiva (2008), Lili
  • Survivre avec les loups (2007)
  • Sans moi (2007), Marie
  • Papa (2005/II), Léa
  • Va, vis et deviens (2005), Yaël Harrari
  • Until Tomorrow Comes (2004), Daughter
  • Alila (2003), Gabi
  • Ballo a tre passi (2003)
  • Haïm Ze Haïm (2003)
  • Miss Entebbe (2003), Elise
  • Bella ciao (2001), Nella
  • Maria, figlia del suo figlio (2000), Mary of Nazareth
  • Kadosh (1999), Rivka
  • Shabatot VeHagim (1999), Ella
  • Passeur d'enfants (1997), Yael
  • L'enfant de la terre promise (1997), Yael
  • L'enfant d'Israel (1997)
  • Hakita Hameofefet (1995)
  • Ha-Yerusha (1993)
  • Zarim Balayla (1993)
  • Sipurei Tel-Aviv (1992), Sharona
  • Pour Sacha (1991), Judith

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yael Abecassis kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.