Vitendawili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Vitendawili ni semi zilizofumbwa ambazo hutolewa kwa hadhira ili zifumbuliwe. Jina linasema kuna pande mbili zinazotenda: anayeuliza na anayeulizwa, ama maneno yalivyo na maana yake ya fumbo.

Fumbo hilo huwa lina mawazo au mafunzo muhimu kwa washiriki na kuchemsha au kufikirisha akili zao.

Vitendawili hufikirisha na kufanya watu wavihusishe na hali halisi ya maisha na vitu au matukio mbalimbali katika mazingira yao na dunia kwa ujumla.

Mifano ya vitendawili ni:

Vitendawili vina utaratibu maalumu vya kuvianza. Mfano:

  • Mtegaji: Kitendawili?
  • Hadhira: Tega.
  • Mtegaji: Popo mbili zavuka mto?
  • Hadhira: miguu.
  • Mtegaji: Mmekosa! nipeni mji.
  • Hadhira: Nenda Mwanza?.
  • Mtegaji: Siendi.
  • Hadhira: Nenda kagera?
  • Mtegaji: Naenda, jibu lake ni macho.

Mwingine:

  • Mtegaji: Mzazi ana miguu, mzaliwa hana.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vitendawili kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.