Urika wa maaskofu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Urika wa maaskofu ni msamiati wa teolojia ambao unatokeza imani ya Kanisa katika umoja wa sakramenti ya daraja takatifu katika ngazi yake ya juu kuhusu utekelezaji wa kazi tatu ambazo Yesu aliwaachia Mitume wake na waandamizi wao kwa njia yao.

Maaskofu wote wanaunda kundi hilo kutokana na sakramenti waliyopokea, hata wasipoongoza jimbo lolote.

Katika Kanisa Katoliki[hariri | hariri chanzo]

Katika utekelezaji wake, Kanisa Katoliki linadai daima uwepo wa mkuu wa kundi la maaskofu, yaani askofu wa Roma akiwa mwandamizi wa mtume Petro ("collegialitas cum et sub Petro").

Fundisho hilo, lililosisitizwa na Mtaguso wa pili wa Vatikano, linatekelezwa hasa maaskofu wanapokutana katika Mtaguso mkuu, lakini pia katika Sinodi ya maaskofu na miundo mingine ya ushirikiano.

Yanayohusu urika wa maaskofu katika Mkusanyo wa Sheria za Kanisa la Kilatini wa mwaka 1983 yanapatikana katika kitabu II, sehemu II, kanuni 336-341.

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Urika wa maaskofu kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.