Tsar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tsar wa mwisho: Nikolai II wa Urusi

Tsar ilikuwa cheo cha mfalme au mfalme mkuu katika Urusi na pia katika Serbia na Bulgaria.

Asili ya neno ni Julius Caesar aliyekuwa kiongozi wa Dola la Roma hadi kuuawa kwake na wapinzani mwaka 44 KK. Watawala waliomfuata walianza kutumia jina la Caesar kwa heshima yake hadi jina lilikuwa cheo. Cheo cha "Caesar" likawa "kaisar" kwa lugha ya Kigiriki na kuingia katika lugha za nchi zilizojaribu kuendeleza Dola la Roma:

  • "Tsar" wa Urusi tangu 1453 baada ya mwisho wa Milki ya Bizanti iliyokuwa mabaki ya Dola la Roma; baada ya Waosmani kuteka mji wa Konstantinopoli mtawala wa Utusi alimwoa binto wa Kaisari wa mwisho wa Bizanti akajitangaza kama mfuasi wake na Moscow kuwa "Roma ya tatu".

Tsar wa mwisho alikuwa mtawala wa Urusi Nikolai II aliyepinduliwa katika mapinduzi ya Urusi ya 1917.