Shajara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Shajara ya kale mwaka 1787

Shajara (kwa lugha ya Kiingereza: diary) ni kitabu maalumu ambamo mwandishi huandika matukio ya kila siku au ya muda fulani.

Shajara ya kibinafsi huenda ikawa na mawazo ya mwandishi; yaliyompata kwa siku na maazimio yake ya siku zijazo.

Kando na shajara ya kibinafsi, kuna shajara rasmi kama za mashirika ("Logbook") ambazo huonyesha matukio ya shirika hilo. Aidha, kabla ya wanafunzi kuhitimu katika kozi zao, wao huenda kwa Kiambatisho Cha Viwanda (Industrial Attachment) na wanahitajika kuandika matukio ya kila siku kwa muda wa miezi mitatu hivi katika Shajara.

Wahasibu pia huwa na shajara ambamo hurekodi kiwango cha pesa walizotumia kununua vitu au zile ambazo zimeingia kwa shirika.

Mti wa Shajara: Mara nyingi, "shajara" inaweza kutumika kumaanisha mti, hasa mti wa pekee au muhimu. Katika baadhi ya lugha, "shajara" inaweza kutumika kumaanisha mti wa matunda au mti unaoheshimiwa kwa namna fulani.

Mzizi wa Familia: Katika muktadha wa ukoo au nasaba, "shajara" inaweza kumaanisha mzizi wa familia au orodha ya watu wa familia na nasaba zao. Historia au Uthibitisho:

"Shajara" inaweza kutumika pia kumaanisha historia au orodha ya matukio na watu. Kwa mfano, "shajara ya matukio" inaweza kumaanisha orodha ya matukio yaliyotokea.