Roko wa Montpellier

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtakatifu Roko alivyochorwa na Francesco Francia.

Roko wa Montpellier (Montpellier, Ufaransa, 1348 hivi - Voghera, Italia, 16 Agosti 1379) alikuwa Mkristo maarufu kwa kuishi miaka mingi bila makao maalumu. Ndiyo maana kwa kawaida anachorwa amevaa nguo za hija.

Katika mizunguko yake sehemu mbalimbali alihudumia kishujaa waliopatwa na tauni na kuwaponya wengi kwa mkono wake wenye karama. Huko Piacenza mwenyewe aliugua tauni akapona.

Miaka 3-5 ya mwisho alikuwa mfungwa gerezani akidhaniwa mpelelezi, asifanye chochote kwa kujitetea au kujitambulisha kwa watawala ambao walikuwa ndugu zake wakamtambua baada ya kufa tu.

Tangu kale ni kati ya watakatifu maarufu zaidi duniani, pia kwa sababu ya miujiza iliyosemekana alifanya wakati wa uhai wake na baada ya kifo, hasa kwa wagonjwa wa tauni, kama alivyoahidi kwa maandishi.

Sikukuu yake ni tarehe 16 Agosti[1].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.