Pepe Reina

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pepe Reina.

Pepe Reina (alizaliwa 31 Agosti 1982) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa timu ya taifa ya Hispania na klabu ya A.C. Milan ya nchini Italia anayecheza katika nafasi ya golikipa.

Reina alianza kuichezea klabu ya Barcelona F.C. ya nchini Hispania na mwaka 2002 alihamia klabu ya Villarreal ya nchini humohumo Hispania.

Mwaka 2005 alihamia klabu ya Liverpool F.C. ya nchini Uingereza na kufanikiwa kushinda taji la UEFA la msimu wa mwa 2005.

Mwaka 2013 Reina alienda kwa mkopo katika klabu ya Napoli ya nchini Italia.

Mwaka 2014 alihamia klabu ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani.

Mwaka 2015 Reina alirudi Napoli na kuichezea mpaka mwaka 2018 ambapo amesajiliwa na klabu ya A.C. Milan.


Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pepe Reina kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.