Nyungunyungu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Anelidi
Nyungunyungu
Nyungunyungu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Nusuhimaya: Eumetazoa (Wanyama wenye tishu za kweli)
Faila ya juu: Lophotrochozoa
Faila: Annelida (Wanyama kama nyungunyungu)
Ngeli: Clitellata
Nusungeli: Oligochaeta
Oda: Megadrilacea
Nusuoda: Lumbricina + Moniligastrida
Ngazi za chini

Familia 21:

Nyungunyungu ni wanyama wadogo wenye umbo la neli wa oda Megadrilacea katika faila Annelida.

Kwa kawaida huishi katika udongo akijilisha kwa viumbehai na waliokufa.

Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula wa nyungunyungu unanyumbua kupitia urefu wa mwili wake, na anaendesha upumuaji kupitia ngozi yake.

Mfumo wa kupeleka viowevu ni maradufu na una uvungu wa mwili (silomi) ambao ndani yake giligili ya silomi inazunguka na mfumo duni wa mzunguko wa damu wenye mtiririko kamili.

Nyungunyungu wana mfumo wa neva wa kati ambao una ganglia mbili juu ya mdomo.

Nyungunyungu ni mahuntha na hubeba ogani zote za kiume na za kike. Hawana mifupa, lakini hudumisha muundo wa mwili kwa njia ya vyumba vya silomi vilivyojaa na giligili na ambavyo hufanya kazi ya kiunzi cha mtuamomaji.

Familia zinazotokea Afrika[hariri | hariri chanzo]

  • Acanthodrilidae
  • Almidae
  • Enchytraeidae
  • Eudrilidae
  • Kynotidae
  • Microchaetidae
  • Ocnerodrilidae
  • Octochaetidae