Mjusi-islam

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mjusi-islam
Jozi ya magonda mdomo-vidoa wakipandana (Trachylepis maculilabris)
Jozi ya magonda mdomo-vidoa wakipandana (Trachylepis maculilabris)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Lacertilia (Mijusi)
Familia ya juu: Scincoidea (Mijusi kama mijusi-islam)
Familia: Scincidae
Ngazi za chini

Nusufamilia 3:

  • Acontinae
  • Lygosominae
  • Scincinae

Mijusi-islam ni mijusi wa familia Scincidae walio na ngozi laini inayong'aa. Spishi za jenasi Trachylepis huitwa magonda pia. Miguu ya mijusi hawa ni mifupi kwa kawaida na spishi nyingi zina miguu iliyopunguka au hazina miguu. Spishi hizi husongea kama nyoka.

Mijusi hawa ni wafupi (sm 5-6) hadi warefu kiasi (sm 60). Huishi kati ya mawe na miamba, katika vishimo, chini ya mchanga au takataka ya majani au juu ya miti. Chakula chao ni wadudu hasa lakini nyungunyungu, majongoo, konokono, mijusi wengine au vipanya pia.

Spishi zilizochaguliwa za Afrika ya Mashariki[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mjusi-islam kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.