Marumaru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uchoraji asilia waonekana kwenye uso wa marumaru iliyokatwa na kusuguliwa.
Sanamu ya marumaru yamwonesha Venus, mungu jike wa Kiroma.

Marumaru (pia: marmar - kutoka Kiarabu مرمر; kwa Kiingereza: marble) ni mwamba wa gange uliobadilika kutokana na joto na shindikizo ndani ya ganda la dunia katika kipindi cha miaka milioni kadhaa. Kikemia ni hasa CaCO3.

Ni jiwe gumu sana linalopatikana katika rangi mbalimbali.

Hupendwa sana kama jiwe la ujenzi, hasa kama ni nyeupe. Kama ni haba katika eneo fulani hutumiwa kama mapambo tu, kama vile kwa kufunika kuta.

Jiwe lenye rangi mbalimbali hutumiwa kwa sakafu katika majengo muhimu au kama mapambo ya kuta za ndani.

Tangu kale marumaru ilitumiwa pia kwa kuchonga sanamu.

Tovuti za nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Marumaru kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.