Maria Zhao Guozhi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wafiadini Wakatoliki wa China.

Maria Zhao Guozhi (Zhaojia, 1840 hivi - Zhaojia, mnamo Julai 1900) alikuwa mwanamke wa China aliyefia Ukristo wakati wa Uasi wa Waboksa.

Pamoja na mabinti wake Roza Zhao na Maria Zhao alijitupa kisimani wasije wakabakwa, lakini walitolewa nje, wakauawa na kuchomwa moto[1]

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu pamoja na wengine 119 tarehe 1 Oktoba 2000.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 9 Julai, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 20 Julai[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.