Kani nje

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kani nje (kwa Kiingereza: centrifugal force) ni kani inayotokea katika mfumo wa mzunguko na kuelekea nje. Inasababishwa na inesha ya masi ya kitu kilichopo katika mwendo wa mzunguko. Katika mzunguko mfululizo ni sawa na kani kitovu.

Katika maisha ya kila siku tunasikia kani nje tukitumia chombo cha usafiri. Tukiwa tumesimama katika basi linalopiga kona tunasikia jinsi gani mwili wetu unavyosukumwa upande wa nje. Kama gari linapita kona kwa kasi kidogo, vitu au mizigo inaweza kuanguka.

Kwa mfano: sayari inayozunguka Jua huwa na obiti thabiti kama kani nje ya mwendo wake ni sawa na kani ya graviti inayoivuta kuelekea Jua. Satelaiti inayopelekwa kwenye obiti ya Dunia inahitaji kurekebisha kasi yake hadi kufikia kani nje inayolingana na graviti ya Dunia.

Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kani nje kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.