Hope & Faith

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hope & Faith

Nembo ya Hope & Faith
Aina Mchezo wa kuchekesha
Imetungwa na Joanna Johnson
Nchi inayotoka Marekani
Lugha Kiingereza
Ina misimu 3
Utayarishaji
Muda makisio ni dk. 30
Urushaji wa matangazo
Kituo ABC
Inarushwa na 26 Septemba 2003
Viungo vya nje

Hope & Faith ni kipindi cha kuchekesha cha Marekani iliyoonyeshwa kuanzia 26 Septemba 2003 hadi 2 Mei 2006 kwa misimu mitatu kwenye stesheni ya ABC.

Kipindi hiki kilikuwa na waigizaji wakuu: Faith Ford na Kelly Ripa. Hope Shanowski (Ford) alikuwa na mume na watoto watatu. Faith Fairfield (Ripa) alikuwa muigizaji maarufu na nduguye Hope. Kipindi hiki inatokana na maisha ya mbunifu Joanna Johnson - ambaye alikuwa mhusika katika kipindi maarufu cha The Bold and the Beautiful. Kipindi hiki kilishirikisha wasanii wengine kama Tony Curtis, Dean Cain, Robert Wagner, Regis Philbin, Kathie Lee Gifford, Jenny McCarthy, Jaclyn Smith, Louise McCafferty na Mark Consuelos.

Kipindi hiki kilirekodiwa mjini New York City kwenye Silvercup Studios.

Mafanikio yake[hariri | hariri chanzo]

Msimu Vipindi Ilianza Ilimalizika Watazamaji
(in milioni)
Namba
1 2003-2004 25 23 Septemba 2003 14 Mei 2004 8.23[1]
2 2004-2005 26 24 Septemba 2004 6 Mei 2005 6.94[2]
3 2005-2006 22 30 Septemba 2005 2 Mei 2006 5.8[3]

Wahusika Wakuu[hariri | hariri chanzo]

  • Hope Fairfield-Shanowski (Faith Ford). Hope ndiye mama wa familia. Ameolewa na Charley na ana watoto watatu: Sydney, Haley, na Justin. Anapenda kupika na kupanda miti kwenye bustani lake.
  • Faith Fairfield (Kelly Ripa). Faith ni nduguye Hope. Yeye ni mvivu, na anamfanya Hope amtendekeze. Mara kwa mara, anazua vitimbi na kumshirikisha nduguye. Yeye amejaribu kutafuta kazi kama mwigizaji, lakini hakufaulu.
  • Charley Shanowski (Ted McGinley). Charley ni mumewe Hope. Yeye hampendi Faith, na kila mara anajaribu kumfukuza Faith kwenye nyumba. Yeye ni daktari wa meno na anapenda kuangalia michezo.
  • Sydney Shanowski (Nicole Paggi). Sydney ni mtoto wa kwanza wa Hope na Charley. Yeye anampenda Faith zaidi ya mamake.
  • Hayley Shanowski (Macey Cruthird). Hayley ni mwana wa pili wa Hope na Charley. Ni mtoto mwerevu aliyerukishwa hadi darasa la kidato cha pili. Yeye ni mwenye huruma na anapenda wanyama.
  • Justin Shanowski (Jansen Panettiere). Ni mwana wa mwisho. Ni mtoto mwerevu anayempenda babake na Faith sana.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Viewership numbers of primetime programs during the 2003-04 television season". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-02-08. Iliwekwa mnamo 2010-01-28.  Retrieved on 2007-11-06.
  2. "Season Program Rankings from 09/20/04 through 05/22/06". ABC Medianet. 24 Mei 2005. Iliwekwa mnamo 2009-07-03. 
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-12-08. Iliwekwa mnamo 2006-12-08.  Unknown parameter |= ignored (help); Unknown parameter |https://web.archive.org/web/20061208201731/http://www.hollywoodreporter.com/hr/search/article_display.jsp?vnu_content_id= ignored (help)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]