Fransisko Maria wa Camporosso

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya Fransisko Maria karibu na Camporosso.

Fransisko Maria wa Camporosso, O.F.M.Cap. (Camporosso 1804 - Genova 1866) alikuwa mtawa ombaomba wa shirika la Ndugu Wadogo Wakapuchini kutoka mkoa wa Liguria nchini Italia.

Alipata umaarufu mjini Genova kwa upendo wake katika kuombaomba mitaani kwa ajili ya shirika lake na ya mafukara aliowatembelea na kuwaombea.

Hatimaye alijitoa mhanga ili kipindupindu mjini kikome ikawa hivyo.

Alitangazwa na Papa Pius XI kuwa mwenye heri tarehe 30 Juni 1929, halafu Papa Yohane XXIII akamtangaza mtakatifu tarehe 9 Desemba 1962.

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 17 Septemba[1].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.