Entebbe

Majiranukta: 0°02′40″N 32°27′57″E / 0.04444°N 32.46583°E / 0.04444; 32.46583
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Jiji la Entebbe
Jiji la Entebbe is located in Uganda
Jiji la Entebbe
Jiji la Entebbe

Mahali pa mji wa Entebbe katika Uganda

Majiranukta: 0°02′40″N 32°27′57″E / 0.04444°N 32.46583°E / 0.04444; 32.46583
Nchi Uganda
Mkoa Kati
Wilaya Wakiso
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 70,200

Entebbe ni mji nchini Uganda. Wakati mmoja, mji huu ulikuwa ngome ya serikali kwa eneo la Uganda, kabla ya Uhuru mwaka wa 1962. Entebbe ndiko eneo la Entebbe International Airport, uwanja wa ndege mkubwa wa Uganda wa kibiashara na kijeshi.Uwanja huu unajulikana kwa shughuli ya kishindo ya kuwaokoa mateka 100 waliotekwa nyara na kundi za kigaidiza PFLP na Revolutionary Cells (RZ).

Mahali[hariri | hariri chanzo]

Entebbe iko 00.04N, 320.280E. Ipo katika wilaya ya Wakiso, kilometre 37 (mi 23) kusini magharibi ya Kampala, mji mkubwa na mji mkuu wa Uganda. Entebbe ipo kaskazini mwa fuo za Ziwa Victoria, ziwa lenye ukubwa zaidi Afrika.

Manispaa iko katika kisiwa kidogo kwenye Ziwa Victoria na eneo jumla la square kilometre 56.2 (sq mi 21.7) kati yake ambayo square kilometre 20 (sq mi 7.7) ni maji. [1] [2]

Idadi ya Watu[hariri | hariri chanzo]

Katika sensa ya kitaifa ya mwaka 2002, idadi ya wakaazi wa Entebbe ilikadiriwa kuwa watu 55,086. Mwaka 2008, Uganda Bureau of Statistics ilikadiriwa idadi ya wakaazi wa mji huu kuwa 70,200. [3]

Historia[hariri | hariri chanzo]

"Entebbe", katika lugha ya Kiganda inamaanisha "kiti " na pengine hi kwa sababu palikuwa mahali ambapo alikaa chifu wa Bagandakuhakimu kesi za kisheria. Ilikuja kuwa eneo la utawala wa kikoloni na kituo cha kibiashara ya Uingereza kwanza mnamo mwaka wa 1893 wakati Sir Gerald Portal, komishona wa kikoloni, aliitumia kama kambi. Port Bell kisha ikawa bandari ya Kampala. Ingawa hakuna meli inayotua nanga huko sasa, bado kuna jetty ambayo ilikuwa ikitumiwa na feri zaZiwa Victoria. Labda Entebbe inafahamika Ulaya kama eneo kuliko na Entebbe International Airport, uwanja wa ndege mkuu wa kimataifa wa Uganda, ambao ulianzishwa mwaka 1947. Uwanja wa ndege wa Entebbe ulikuwa mahali ambapo oparesheni moja ya kusisimua wakati kitengo cha wanajeshi wa jeshi la Israel waliwaokoa mateka zaidi ya 100 kufuatia utekaji nyara na kundi la Wapalestina na magaidi wa Kijerumani. Ilikuwa pia kutoka uwanja wa ndege huu Malkia Elizabeth II aliondoka kutoka Afrika kurejea Uingereza mwaka Malkia.

Maeneo ya kitalii[hariri | hariri chanzo]

  • Bustani kuu za kitaifa zilizowekwa mwaka wa 1898, ziko katika Entebbe.
  • Entebbe nyumbani mwa Uganda Virus Research Institute (UVRI).
  • Entebbe kuna Uganda Wildlife Education Center (UWEC), pia inatumika kama mbuga ya kitaifa. Mlango wa kituo iko karibu na jetty. Watalii wa kigeni wamebaini nyani wa mwituni wakiwa wameketi juu ya miti kwenye njia ya kituo hiki.
  • Entebbe ni eneo la Chuo Kikuu cha Nkumba, mojawapo ya taasisi thelathini na moja (31) za elimu ya juu zilizo pewa leseni nchini Uganda.
  • Entebbe pia ni eneo la State House, makazi rasmi ya Rais wa Uganda [4]

Picha[hariri | hariri chanzo]

Maeneo mengine muhimu[hariri | hariri chanzo]

Maeneo mengine muhimu yapo kando kando mwa mji huu na ni kama:

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. [5] ^ Location of Entebbe
  2. [6] ^Distance from Kampala to Entebbe with Map
  3. [7] ^ 2002 and 2008 Estimated Populations of Uganda Cities and Towns
  4. "State House, Entebbe". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-06-05. Iliwekwa mnamo 2009-12-05. 
  5. [10] ^ Bank of Africa Opens Entebbe Branch

0°02′40″N 32°27′57″E / 0.04444°N 32.46583°E / 0.04444; 32.46583