Dawati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Madawati darasani nchini Madagaska
Dawati la shule kwenye makumbusho nchini Norwei.

Dawati (kutoka neno la Kiarabu; pia deski[1] kutoka neno la Kiingereza desk) ni meza inayotumiwa hasa na mwanafunzi kwa kuandikia au kusomea mara nyingi ikiwa na sanduku la kuwekea vitabu, madaftari na kalamu.

Madawati ya shule mara nyingi hutengenezwa pamoja na kiti chake kama kipande kimoja, ilhali kimo cha sehemu ya meza na ya kiti hulingana na umri wa wanafunzi wanaolengwa. Upana wa dawati hutengenezwa kulingana na idadi ya watu wanaokaa katika dawati hilo. Kuna dawati la mtu mmoja watu wawili na watu watatu.

Madawati hupatikana shuleni, ofisini, nyumbani na kadhalika.

Wakati mwingine dawati linataja mtoto wa meza au saraka pekee.

Kwa maana tofauti kidogo "dawati" linaweza kumaanisha pia ofisi, kitengo au idara ndani ya taasisi fulani; kwa mfano "dawati la vijana" linaweza kutaja afisa au maafisa wanaohusika na mambo ya vijana katika ofisi kuu ya chama.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Kufuatana na Kamusi Kuu dawati na deski ni visawe