Dado

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya Mt. Audoin (kushoto) na Mt. Waninge (kulia), huko Fécamp, Ufaransa.

Dado (pia: Audoin, Audoen, Owen na Ouen wa Rouen; Sancy, Ufaransa, 609Clichy, Ufaransa, 686)[1][2][3] alikuwa askofu na waziri wa Wafaranki.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 24 Agosti[4].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Mtoto wa mtakatifu Authaire (Audecharius), alilelewa katika ikulu ya mfalme Chlothar II (aliyefariki 629), ambapo alipata elimu na uanajeshi pamoja na vijana wengine wa koo maarufu.

Baadaye alisimamia mali ya Dagobert I[5], akishika sana maadili[6] na akiwa na marafiki kama watakatifu Wandregisel, Didier wa Cahors na Eligius, ambaye Ouen aliandika habari za maisha yake.

Mwaka 635 pamoja na ndugu zake Ado na Rado alianzisha abasia ya Rebais, halafu monasteri ya Mt. Wandrille huko Rouen, na nyingine ya kike huko Fécamp. Fredegar reports that even as court referendary, Audoin had a reputation of being a religious man.

Mwaka 641 alifanywa askofu wa Rouen.[5]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Vyanzo[hariri | hariri chanzo]

  • Alban Butler's Lives of the Saints, edited, revised and supplemented by Thurston and Attwater - Christian classics, Westminster, Maryland.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.