Busia, Uganda

Majiranukta: 00°28′01″N 34°05′20″E / 0.46694°N 34.08889°E / 0.46694; 34.08889
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Busia
Busia is located in Uganda
Busia
Busia

Mahali pa mji wa Busia katika Uganda

Majiranukta: 00°28′01″N 34°05′20″E / 0.46694°N 34.08889°E / 0.46694; 34.08889
Nchi Uganda
Mkoa Mashariki
Wilaya Busia
Serikali
 - Mayor Michael Mungeni
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 43,200
Busia,Uganda
Ramani ya Busia,Uganda

Busia ni mji katika mashariki mwa Uganda. Huu ndio mji mkubwa katika Wilaya ya Busia na makao makuu ya wilaya yako hapo.

Mahali[hariri | hariri chanzo]

Busia iko kwenye mpaka na Kenya. Mji huu ni takriban kilometre 202 (mi 126) kwa barabara, mashariki kwa Kampala, jiji kubwa na mji mkuu wa Uganda. [1]

Idadi ya Watu[hariri | hariri chanzo]

Katika mwaka 2002, sensa ya kitaifa ilihesabu idadi ya wakazi Busia, Uganda, kuwa 36,630. Mwaka 2008, Uganda Bureau of Statistics ilikadiria idadi ya wakazi wa mji huu kuwa 43,200. [2]

Shughuli za Kiuchumi[hariri | hariri chanzo]

Mji huu, pamoja na mji dada yake wa Busia, Kenya kando ya mpaka, ni vituo vya shughuli za biashara kubwa na trafiki ni nzito katika pande zote mbili. Bidhaa kutoka Uganda ni pamoja na mazao ya biashara kama kahawa, pamba na mbao zinazopelekwa katika bandari ya Mombasa nchini Kenya kwa ajili ya kuuza nje. Vyakula kama ndizi, mananasi na maembe zinazopelekwa kwa soko ya Kenya pia hupita mpakani. Kwa upande mwingine, Uganda huagiza mafuta ya petroli, bidhaa za viwandani na nyumbani kama mafuta ya kupikia, sabuni, nguo,vifaa vya elektronik na magari.

Busia ndio mji wa shughuli nyingi sana mpakani kati ya nchi hizi mbili jirani wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mji wa mpaka wa Malaba ulioko takribani kilometre 46 (mi 29) kaskazini, ni wa pili kwa shughuli za biashara kati ya Uganda na Kenya katika eneo la pamoja la mpaka wao. Tazama jadwali hapa chini:

Kiwango cha biashara kwa miji iliyoko kwenye mpaka za Uganda mwaka 2005
Nambari Mji ulioko mpakani Kiwango cha mauzo ya kutoka Kiwango cha mauzo ya kuingia
1 Busia 42.7% 54.3%
2 Mpondwe 25.0% 10.6%
3 Malaba 7.8% 19.9%
4 Paidha 9.3% 2.2%
5 Mingine 15.2% 13.0%
Jumla 100.0% 100.0%

Alama za Umuhimu[hariri | hariri chanzo]

Alama zilizoko ndani ya mji huu au karibu na mipaka yake ni pamoja na:

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Angalia Pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Distance between Kampala and Busia with Map
  2. 2002 and 2008 Estimated Populations of Uganda Cities and Towns


00°28′01″N 34°05′20″E / 0.46694°N 34.08889°E / 0.46694; 34.08889