Bergisch Gladbach

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mji wa Bergisch Gladbach


Bergisch Gladbach
Bergisch Gladbach is located in Ujerumani
Bergisch Gladbach
Bergisch Gladbach

Mahali pake katika Ujerumani

Majiranukta: 51°06′00″N 07°07′00″E / 51.10000°N 7.11667°E / 51.10000; 7.11667
Nchi Ujerumani
Jimbo Rhine Kaskazini-Westfalia
Idadi ya wakazi (2009)
 - Wakazi kwa ujumla 105,699
Tovuti:  http://www.bergischgladbach.de/

Bergisch Gladbach ni mji uliopo nchini Ujerumani katika jimbo la Rhine Kaskazini-Westfalia. Mji upo karibu na mji wa Cologne na una wakazi takriban 110,016 waishio katika mji huo.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Mji wa Bergisch Gladbach upo mjini mashariki mwa Mto Rhine, kilomita kumi mashariki kwa mji wa Cologne.

Manispaa jirani za mji huu[hariri | hariri chanzo]

Kwa kuanzia kaskazini mwa mji huu, miji ya jirani na mji huu ni: Odenthal, Kürten, Overath, Rösrath, Cologne na Leverkusen.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Makazi ya awali yalianza tangu kunako karne ya 13, lakini mji ulitambuliwa rasmi mnamo mwaka wa 1856.

Ngoma ya kale ya mjini Bensberg.

Neno “Bergisch” linatokana na asili ya eneo lake la Berg na ulipangwa kuondolewa katika Mönchengladbach. Mnamo mwaka wa 1975, mji huu ukishirikiana na mji wa jirani yake wa Bensberg na ulipofikia idadi ya watu 100,000 mnamo 1977 ukapewa heshima kuwa jiji.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Makala hii kuhusu maeneo ya Ujerumani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bergisch Gladbach kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.