Basiano wa Lodi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Basiano.

Basiano wa Lodi (kwa Kilatini: Bassianus; 310 hivi - Siracusa, Sicilia, Italia, 19 Januari 409) alikuwa askofu wa mji huo wa Italia Kaskazini kuanzia mwaka 373 hadi kifo chake.

Kama kijana alikwenda Roma kwa masomo, na huko aliongokea dini ya Ukristo. Baba yake alitaka aasi na kurudi nyumbani, lakini yeye alikataa na kukimbilia Ravenna.

Baada ya kuchaguliwa askofu, alishiriki mtaguso wa Akwileia (381) na labda hata mtaguso wa Milano (390). Ili kulinda kundi lake dhidi ya uzushi wa Ario, uliokuwa bado na nguvu katika eneo hilo, alipambana kwa bidii pamoja na rafiki yake askofu Ambrosi wa Milano. Pamoja naye alisaini barua kwa Papa Sirisi.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Januari[1].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.