Bahari ya Sulu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bahari ya Sulu kati ya Borneo na Ufilipino.
Papa anayepatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Twanga ya Tubbataha, Bahari la Sulu, Ufilipino.

Bahari ya Sulu (kwa Kifilipino; Dagat ng Sulu; kwa Kiingereza: Sulu Sea) ni sehemu ya Bahari Pasifiki iliyopo kati ya Ufilipino na kaskazini mashariki mwa kisiwa cha Borneo (sehemu ya Malaysia), ikipakana upande moja na funguvisiwa la Sulu (ng'ambo yake Bahari ya Celebes) na kwa upande wa kaskazini mashariki na kisiwa cha Palawan (ng'ambo yake Bahari ya Kusini ya China). [1] [2]

Jiografia na ekolojia[hariri | hariri chanzo]

Uso wa sehemu hii ya bahari ina kilomita za mraba 260,000. Kina cha wastani ni mita 1139.

Ndani ya Bahari ya Sulu iko Hifadhi ya Taifa ya Tubbataha Reef iliyoorodheshwa na UNESCO kati ya Urithi wa Dunia. [3]

Kusini magharibi mwa Bahari ya Sulu kuna visiwa ambako kasa wanatega mayai yao, hasa Kasa Uziwa (chelonia mydas) na Kasa Mwamba (eretmochelys imbricata).

Maharamia[hariri | hariri chanzo]

Bahari ya Sulu ina historia ndefu ya uharamia uliostawi katika mapambano baina ya Wahispania (waliotawala sehemu za visiwa vya Ufilipino) na wapinzani wao wazalendo.

Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia uharamia ulipata nguvu tena. Mara nyingi ni makundi ya maharamia hadi kumi wanaoshambulia hasa maboti madogo ya mizigo na ya abiria pamoja na wavuvi. Katika miaka ya 1980 takriban mashambulio 100 yalikadiriwa kila mwaka katika Bahari ya Sulu.[4]:60 Maharamia wa eneo hili wanahofiwa kwa sababu wanaua haraka kuliko kawaida na pia wanateka nyara.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Coron Bay, Philippines : UnderwaterAsia.info. www.underwaterasia.info. Jalada kutoka ya awali juu ya 5 October 2017. Iliwekwa mnamo 23 April 2018.
  2. Sulu Sea, Philippines : UnderwaterAsia.info. www.underwaterasia.info. Jalada kutoka ya awali juu ya 1 June 2016. Iliwekwa mnamo 23 April 2018.
  3. C.Michael Hogan. 2011. Sulu Sea. Encyclopedia of Earth. Eds. P.Saundry & C.J.Cleveland. Washington DC
  4. Liss, Carolin (2011). Oceans of Crime. Maritime Piracy and Transnational Security in Southeast Asia and Bangladesh. Singapore: ISEAS Publishing. ISBN 978-981-4279-46-8. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bahari ya Sulu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.