Bernardino wa Siena : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
+img
Mstari 17: Mstari 17:
== Heshima baada ya kifo ==
== Heshima baada ya kifo ==
Kutokana na sifa yake kubwa, alitangazwa [[mtakatifu]] na [[Papa Nikolasi V]] mwaka [[1450]]. Kumbukumbu yake inaadhimishwa kila tarehe [[20 Mei]].
Kutokana na sifa yake kubwa, alitangazwa [[mtakatifu]] na [[Papa Nikolasi V]] mwaka [[1450]]. Kumbukumbu yake inaadhimishwa kila tarehe [[20 Mei]].

==Tazama pia==
*[[Watakatifu wa Agano la Kale]]
*[[Orodha ya Watakatifu Wakristo]]
*[[Orodha ya Watakatifu Wafransisko]]


== Marejeo ==
== Marejeo ==

Pitio la 07:09, 14 Mei 2017

Pinturicchio (1486), Utukufu wa Mt. Bernardino da Siena, Roma, kanisa la Santa Maria in Aracoeli
Della confessione regole 12., 1494

Bernardino wa Siena (8 Septemba 1380 - 20 Mei 1444) alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo na kasisi wa Kanisa Katoliki.

Maisha ya awali

Alizaliwa na kubatizwa Massa Marittima (Siena) tarehe 8 Septemba 1380 katika familia Albizzeschi kutoka Siena, ambako alihamia baada ya kubaki yatima, ili alelewe na ndugu zake na kusomeshwa.

Wito na utume

Akiwa na miaka 22, alijiunga na utawa, katika tawi la urekebisho wa Waobservanti, ambalo akawa nguzo yake kuu, pamoja na Yohane wa Kapestrano, Yakobo wa Marka na Alberto wa Sarteano.

Kisha akaanza utume mkubwa akihubiri kwa mafanikio katika Italia Kaskazini. Kazi yake yaliamsha katika Kanisa imani na ibada kwa Jina la Yesu na kurekebisha maadili ya wengi. Ndiye aliyesambaza kila mahali vibao vyenye kifupisho JHS (Jesus Hominum Salvator) kikiwa na msalaba juu yake na kuzungukwa na jua lenye miali 12.

Kifo

Alifariki huko L'Aquila, tarehe 20 Mei 1444.

Heshima baada ya kifo

Kutokana na sifa yake kubwa, alitangazwa mtakatifu na Papa Nikolasi V mwaka 1450. Kumbukumbu yake inaadhimishwa kila tarehe 20 Mei.

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu: