Mtume Barnaba : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Mstari 26: Mstari 26:


Wataalamu wengine wanamtaja kama [[mtunzi]] wa [[Waraka kwa Waebrania]], na [[Klemens wa Aleksandria]] alimtaja kama [[mwandishi]] wa [[Waraka wa Barnaba]], lakini hakuna hakika.
Wataalamu wengine wanamtaja kama [[mtunzi]] wa [[Waraka kwa Waebrania]], na [[Klemens wa Aleksandria]] alimtaja kama [[mwandishi]] wa [[Waraka wa Barnaba]], lakini hakuna hakika.

==Tazama pia==
*[[Watakatifu wa Agano la Kale]]
*[[Orodha ya Watakatifu Wakristo]]
*[[Orodha ya Watakatifu Wafransisko]]


==Marejeo==
==Marejeo==

Pitio la 07:01, 14 Mei 2017

Kifodini cha Mt. Barnaba, kutoka Legenda Aurea ya Jacopo wa Varazze.

Mtume Barnaba' (jina la awali Yosefu wa Kupro) alikuwa Myahudi wa kabila la Lawi wa karne ya 1 BK.

Anajulikana hasa kwa jina la Barnaba (kwa Kiaramu בר נביא, bar naḇyā, yaani 'mwana wa nabii'. Lakini Luka mwinjili (kitabu cha Matendo ya Mitume 4:36) alilitafsiri kwa Kigiriki υἱός παρακλήσεως, huios paraklēseōs, yaani "mwana wa faraja" au "mwana wa himizo".

Habari zake katika Biblia

Katika kitabu hicho cha Agano Jipya (Biblia ya Kikristo) tunapata habari kuwa aliongokea mapema Ukristo, akauza shamba lake na kuwakabidhi Mitume wa Yesu mapato yake ili wawasaidie maskini. Labda kwa sababu hiyo Mitume walimuita Barnaba (Mdo 4:36-37).

Kisha kuheshimiwa hivyo katika Kanisa la awali huko Yerusalemu, alimtambulisha na kumdhamini Mtume Paulo muda mfupi baada ya huyo kuongoka huko Damasko (Mdo 9:26Katika kitabu hicho cha Agano Jipya (Biblia ya Kikristo) tunapata habari kuwa aliongokea mapema Ukristo, akauza shamba lake na kuwakabidhi Mitume wa Yesu mapato yake ili wawasaidie maskini. Labda kwa sababu hiyo Mitume walimuita Barnaba (Mdo 4:36-37). -28).

Watu wa mataifa walipoanza kuingizwa moja kwa moja katika Ukristo mjini Antiokia, alitumwa huko kwa niaba ya Kanisa mama, akawa kiongozi mkuu wa jumuia hiyo mpya (Mdo 11:19-30; 13:1).

Baadaye Roho Mtakatifu alidai yeye na Paulo wapelekwe kufanya umisionari sehemu nyingine, wakaondoka pamoja na binamu yake, Yohane Marko, kuelekea kwanza kisiwani Kupro, halafu bara, katika maeneo ya Uturuki Kusini wa leo (Mdo 13:2-14:28).

Kazi yao ilipopata upinzani kwa sababu ya kutodai Wapagani wakiongoka washike Torati yote, walikwenda pamoja Yerusalemu (mwaka 49 hivi, kwa mtaguso wa Mitume, ambao uliamua kuhusu suala hilo (Mdo 15:1-35).

Baada ya kutengana na Paulo, Barnaba alifunga tena safari kwenda Kupro pamoja na Marko (Mdo 15:36-39) kati ya miaka 50 na 53.

Baada ya hapo hatuna tena habari ya hakika juu yake, ila Mtume Paulo alimtaja kama mfano wa mtu asiye na mke kwa ajili ya uinjilishaji (1Kor 9:16-22).

Kilichofuata

Mapokeo yanasema aliuawa kwa ajili ya imani yake huko Salamis, Kupro, mwaka 61.

Kanisa Katoliki, Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki, Waanglikana na Walutheri wanamheshimu kama mtakatifu tarehe 11 Juni.

Wataalamu wengine wanamtaja kama mtunzi wa Waraka kwa Waebrania, na Klemens wa Aleksandria alimtaja kama mwandishi wa Waraka wa Barnaba, lakini hakuna hakika.

Tazama pia

Marejeo

  • Attwater, Donald and Catherine Rachel John. "The Penguin Dictionary of Saints," 3rd edition, New York: Penguin Books, 1993. ISBN 0-14-051312-4.

Kuhusu maandishi yake

  • Die Apostolischen Väter. Griechisch-deutsche Parallelausgabe. J.C.B. Mohr Tübingen 1992. ISBN 3-16-145887-7
  • Der Barnabasbrief. Übersetzt und erklärt von Ferdinand R. Prostmeier. Series: Kommentar zu den Apostolischen Vätern (KAV, Vol. 8). Vandenhoeck & Ruprecht: Göttingen 1999. ISBN 3-525-51683-5

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu: