Masafa ya mawimbi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
No edit summary
d Kipala alihamisha ukurasa wa Urefu wa wimbi hadi Masafa ya mawimbi
(Hakuna tofauti)

Pitio la 14:39, 28 Aprili 2017

Picha inaonyesha mawimbi kwenye bahari; alama ya λ inaonyesha umbali kati ya vilele vya mawimbi mawili au urefu wa wimbi = lukoka.
Lukoka au urefu wa wimbi hupimwa kati ya sehemu zinazolingana ya mawimbi mawili.

Urefu wa wimbi (pia masafa[1], mara chache lukoka[2]; kwa Kiingereza wavelength) ni namna ya kupima na kutaja ukubwa wa wimbi.

Ni umbali kati ya sehemu za kulingana za mawimbi mawili ambayo yanafuatana, kwa mfano kati ya kilele na kilele au mabonde yao.

Mawimbi yapo kila sehemu ya mazingira asilia, kwa mfano:

Urefu wa mawimbi unatofautiana sana. Mawimbi marefu yanayoweza kutambuliwa na milango ya fahamu ya binadamu ni sauti ya besi yenye lukoka ya mita 21. Sikio letu linatambua mawimbi yenye urefu kati ya milimita 17 hadi mita 21.

Mawimbi sumakuumeme yana upeo mkubwa.

Urefu wa wimbi na marudio

Urefu wa wimbi huwa na uhusiano wa kinyume na marudio ya wimbi. Kama marudio ya wimbi ni ya juu, urefu wake ni mdogo. Vilevile kinyume, kama wimbi lina urefu mkubwa, marudio yake ni madogo.

Marejeo

  1. Kamusi ya TUKI
  2. Lukoka ni pendekezo la KAST, 1995 lisilotumika sana

Tovuti za Nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu: