Mshale (kundinyota) : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 18: Mstari 18:


Katika vitabu kadhaa vya shule za msingi nchini Tanzania "Kausi" imetumiwa kwa kosa kutaja [[sayari]] ya nane katika [[mfumo wa jua]] letu yaani [[Neptun]].
Katika vitabu kadhaa vya shule za msingi nchini Tanzania "Kausi" imetumiwa kwa kosa kutaja [[sayari]] ya nane katika [[mfumo wa jua]] letu yaani [[Neptun]].

==Marejeo==
*kuhusu jina: Jan Knappert, The Swahili names of stars, planets and constellations; makala katika jarida la The Indian Ocean Review, Perth, Australia September 1993, uk. 7


[[Jamii:Kundinyota]]
[[Jamii:Kundinyota]]

Pitio la 06:11, 25 Aprili 2017

Kwa habari za sayari ya nane katika mfumo wa jua letu (wakati mwingine kuitwa "Kausi" pia) angalia hapa Neptun

Nyota za Kausi angani (mistari imeongezwa kwenye picha tu)
Kausi (sagittarius) jinsi anavyochorwa na msanii

Kausi ni jina la kundinyota inayojulikana pia kwa jina la Kilatini Sagittarius.

Jina la Kiswahili limetokana na neno la Kiarabu Kaus قوس linalomaanisha "mpiga mishale", maana sawa na jina la "sagittarius". Wataalamu wa kale waliona katika nyota zake picha ya mtu anayekalia juu ya farasi akishika pinde na kulenga mshale.

Jina la "Kaus" limetumiwa pia katika astronomia ya kimagharibi kutaja nyota kadhaa zilizomo hapa kama vile Kaus Australis, Kaus Medius na Kaus Borealis.

Kausi inaonekana pale angani ambako njia nyeupe inang'aa zaidi yaani kuelekea kitovu cha galaksi yetu.

Kausi ni kati ya fungunyota zilizojulikana tangu karne nyingi zikitumiwa hasa na mabaharia kutafuta njia baharini wakati wa usiku.

Katika eneo la Kausi magimba ya angani kadhaa ya maana yalitambuliwa na wanaastronomia. Hizi ni pamoja

  • Sagittarius A ambayo ni chanzo cha mawimbi ya redio; inaaminiwa ya kwamba mawimbi haya ni dalili za kuwepo kwa shimo cheusi kubwa sana
  • Nebula kadhaa zilizoandikishwa katika orodha ya Messier kama vile nebula za lagoon, omega na red spider.

Katika vitabu kadhaa vya shule za msingi nchini Tanzania "Kausi" imetumiwa kwa kosa kutaja sayari ya nane katika mfumo wa jua letu yaani Neptun.

Marejeo

  • kuhusu jina: Jan Knappert, The Swahili names of stars, planets and constellations; makala katika jarida la The Indian Ocean Review, Perth, Australia September 1993, uk. 7