Shahada ya Awali : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
No edit summary
d Kipala alihamisha ukurasa wa Digrii ya bachelor hadi Shahada ya Awali
(Hakuna tofauti)

Pitio la 09:45, 30 Machi 2017

Digrii ya bachelor ni shahada ya kwanza inayotolewa kwa mwanafunzi wa chuo kikuu aliyefaulu masomo ya fani fulani katika muda wa miaka mitatu au minne, kutegemeana na nchi na mfumo wa chuo.

Neno "bachelor" kwa lugha ya Kiingereza kimsingi linataja mtu asiyeoa bado lakini mwenye umri wa kutosha.

Katika nchi zinazofuata mfumo wa Uingereza ni miaka mitatu, kwenye mfumo wa Marekani ni muda wa miaka minne kutokana na tofauti katika kiwango cha elimu ya sekondari.

Nchi nyingine hazina digrii hiyo kwa sababu kwao masomo ya chuo kikuu hupangwa kwa muda wa miaka mitano hadi sita tangu mwanzo.

Vyeo vinavyofuata ni digrii ya uzamili ("masters") na digrii ya uzamifu ("udaktari").