Bastola : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Removing "Pistol_Browning_SFS.jpg", it has been deleted from Commons by Ellin Beltz because: per c:Commons:Deletion requests/File:Pistol Browning SFS.jpg.
picha
Mstari 1: Mstari 1:
[[Picha:Python-nickel.jpg|thumb||Bastola aina za revolver]]
[[Picha:Browning High-Power 9mm IMG 1526.jpg|thumb|Bastola]]
[[Picha:Enfield-No2.jpg|thumb||Bastola aina za revolver]]


'''Bastola''' ni [[silaha ya moto]] ndogo yenye [[kasiba]] fupi inayoshikwa kwa mkono mmoja tu. Teknolijia yake ni karibu sawa na bunduki isipokuwa ni ndogo.
'''Bastola''' ni [[silaha ya moto]] ndogo yenye [[kasiba]] fupi inayoshikwa kwa mkono mmoja tu. Teknolijia yake ni karibu sawa na bunduki isipokuwa ni ndogo.


Mstari 19: Mstari 19:


[[Jamii:Silaha]]
[[Jamii:Silaha]]

[[en:Handgun]]
[[fa:سلاح کمری]]

Pitio la 10:57, 23 Januari 2017

Bastola
Bastola aina za revolver

Bastola ni silaha ya moto ndogo yenye kasiba fupi inayoshikwa kwa mkono mmoja tu. Teknolijia yake ni karibu sawa na bunduki isipokuwa ni ndogo.

Aina za bastola

Kiasili bastola ilikuwa tu umbo dogo la gobori. Baada ya kila pigo ilihitaji kujazwa upya.

Kwa muda bastola zenye kasiba mbili au zaidi zilitengenezwa kwa kusudi la kuongeza kasi ya kufyatulia risasi.

Baada ya kupatikana kwa ramia za metali katika karne ya 19 bastola ilipewa chemba ya risasi inayozunguka. Modeli mashuhuri ya mwanzoni ilikuwa aina ya Colt. Kwa kiingereza aina hii huitwa "revolver" kutokana na mzunguko wa chemba. Chemba huwa na ramia 5-8 mara nyingi ni sita.

Aina ya pili kati ya bastola ina chemba ya risasi kama kidawati kidogo inayosukumwa ndani ya nafasi yake kwenye bastola. Wanajeshi waliona faida ya kwamba ni rahisi kujaza chemba ya ziada na kuibeba kama akiba inayobadilishwa haraka kuliko kujaza upya chemba inayozunguka kwa sababu chemba ya kuzunguka haitolewi ni lazima kuijaza ramia moja-moja.

Matumizi ya bastola na bunduki

Faida yake kulingana na bunduki yenyewe ni nyepesi na ndogo hivyo haisumbui wakati wa kubeba. Hasara yake katika ulinganisho na bunduki ni hasa mfiko mdogo, nguvu ya risasi zake na umakinifu wa kulenga.

Jeshini bastola hutumiwa kama silaha ya pili pamoja na bunduki. Kwa polisi huwa ni silaha kali ya kawaida. Majambazi mara nyingi hupendelea bastola kwa sababu zinafichwa rahisi hazionekani.